Ezra 3:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wajenzi walipoanza kuweka msingi wa hekalu la Mwenyezi-Mungu, makuhani wakiwa wamevalia mavazi yao rasmi, walisimama mahali pao na tarumbeta mikononi, nao Walawi wa ukoo wa Asafu wakisimama na matoazi yao; basi, walimtukuza Mwenyezi-Mungu kufuatana na maagizo ya mfalme Daudi wa Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wajenzi walipoweka msingi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu, makuhani wakiwa wamevalia mavazi yao wakiwa na tarumbeta na Walawi (wana wa Asafu) wakiwa na matoazi, walishika nafasi zao za kumhimidi Mwenyezi Mungu, kama ilivyoagizwa na Daudi mfalme wa Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata wajenzi walipouweka msingi wa hekalu la Bwana, wakawaweka makuhani, wamevaa mavazi yao, wenye baragumu, na Walawi, wana wa Asafu, wenye matoazi, ili wamhimidi Bwana, kama alivyoagiza Daudi, mfalme wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wajenzi walipoanza kuweka msingi wa hekalu la Mwenyezi-Mungu, makuhani wakiwa wamevalia mavazi yao rasmi, walisimama mahali pao na tarumbeta mikononi, nao Walawi wa ukoo wa Asafu wakisimama na matoazi yao; basi, walimtukuza Mwenyezi-Mungu kufuatana na maagizo ya mfalme Daudi wa Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wajenzi walipoweka msingi wa Hekalu la BWANA, makuhani wakiwa wamevalia mavazi yao wakiwa na tarumbeta na Walawi (wana wa Asafu) wakiwa na matoazi, walishika nafasi zao za kumtukuza BWANA, kama ilivyoagizwa na Daudi mfalme wa Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wajenzi walipoweka msingi wa Hekalu la bwana, makuhani wakiwa wamevalia mavazi yao wakiwa na tarumbeta na Walawi (wana wa Asafu) wakiwa na matoazi, walishika nafasi zao za kumtukuza bwana, kama ilivyoagizwa na Daudi mfalme wa Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata wajenzi walipouweka msingi wa hekalu la BWANA, wakawaweka makuhani, wamevaa mavazi yao, wenye baragumu, na Walawi, wana wa Asafu, wenye matoazi, ili wamhimidi BWANA, kama alivyoagiza Daudi, mfalme wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wajenzi walipoanza kuweka msingi wa hekalu la Mwenyezi-Mungu, makuhani wakiwa wamevalia mavazi yao rasmi, walisimama mahali pao na tarumbeta mikononi, nao Walawi wa ukoo wa Asafu wakisimama na matoazi yao; basi, walimtukuza Mwenyezi-Mungu kufuatana na maagizo ya mfalme Daudi wa Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waashi walipoanza kuyapigilia mawe ya misingi ya Jumba la Bwana wakaweka hapo watambikaji waliovikwa mavazi yao, wakishika matarumbeta, nao Walawi waliokuwa wana wa Asafu, wakishika matoazi, wamtukuze Bwana na kumwimbia wimbo wa Dawidi, mfalme wa Isiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata wajenzi walipouweka msingi wa hekalu la BWANA, wakawaweka makuhani, wamevaa mavazi yao, wenye baragumu, na Walawi, wana wa Asafu, wenye matoazi, ili wamhimidi BWANA, kama alivyoagiza Daudi, mfalme wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wajengaji walipoanza kuweka musingi wa hekalu la Yawe, makuhani wakiwa wamevaa nguo zao, walisimama pahali pao na baragumu katika mikono, nao Walawi wa ukoo wa Asafu wakisimama na matoazi yao, basi, wakamutukuza Yawe kufuatana na maagizo ya mufalme Daudi wa Israeli.