Ezra 3:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waliimba kwa kupokezana, wakimsifu na kumtukuza Mwenyezi-Mungu: “Kwa kuwa yu mwema, fadhili zake kwa Israeli zadumu milele.” Watu wote walipaza sauti kwa nguvu zao zote, wakamsifu Mwenyezi-Mungu kwa sababu ya kuanza kujengwa msingi wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waliimba nyimbo za sifa na za shukrani kwa Mwenyezi Mungu hivi: “Yeye ni mwema; upendo wake kwa Israeli wadumu milele.” Watu wote wakapaza sauti kubwa za sifa kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu msingi wa nyumba ya Mwenyezi Mungu ulikuwa umewekwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaimbiana, wakimhimidi Bwana, na kumshukuru, wakasema, Kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake kwa Israeli ni za milele. Kisha watu wote wakapaza sauti zao, na kupiga kelele, walipomhimidi Bwana, kwa sababu msingi wa nyumba ya Bwana umekwisha kuwekwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waliimba kwa kupokezana, wakimsifu na kumtukuza Mwenyezi-Mungu: “Kwa kuwa yu mwema, fadhili zake kwa Israeli zadumu milele.” Watu wote walipaza sauti kwa nguvu zao zote, wakamsifu Mwenyezi-Mungu kwa sababu ya kuanza kujengwa msingi wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waliimba nyimbo za sifa na za shukrani kwa BWANA hivi: “Yeye ni mwema; upendo wake kwa Israeli wadumu milele.” Watu wote wakapaza sauti kubwa za sifa kwa BWANA, kwa sababu msingi wa nyumba ya BWANA ulikuwa umewekwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waliimba nyimbo za sifa na za shukrani kwa bwana hivi: “Yeye ni mwema; upendo wake kwa Israeli wadumu milele.” Watu wote wakapaza sauti kubwa za sifa kwa bwana, kwa sababu msingi wa nyumba ya bwana ulikuwa umewekwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaimbiana, wakimhimidi BWANA, na kumshukuru, wakasema, Kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake kwa Israeli ni za milele. Kisha watu wote wakapaza sauti zao, na kupiga kelele, walipomhimidi BWANA, kwa sababu msingi wa nyumba ya BWANA umekwisha kuwekwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waliimba kwa kupokezana, wakimsifu na kumtukuza Mwenyezi-Mungu: “Kwa kuwa yu mwema, fadhili zake kwa Israeli zadumu milele.” Watu wote walipaza sauti kwa nguvu zao zote, wakamsifu Mwenyezi-Mungu kwa sababu ya kuanza kujengwa msingi wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaitikiana na kumtukuza na kumshukuru Bwana kwamba: Bwana ni mwema, upole wake ni wa kale na kale, nao huwakalia Waisiraeli. Nao watu wote pia wakapaza sana sauti za kupiga shangwe, wamtukuze Bwana, kwa kuwa misingi ya Nyumba ya Bwana iliwekwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaimbiana, wakimhimidi BWANA, na kumshukuru, wakasema, Kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake kwa Israeli ni za milele. Kisha watu wote wakapaza sauti zao, na kupiga kelele, walipomhimidi BWANA, kwa sababu msingi wa nyumba ya BWANA umekwisha kuwekwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakaimba kwa kupokezana, wakimusifu na kumutukuza Yawe: “Yeye ni muzuri, wema wake kwa Waisraeli unadumu milele.” Watu wote walipaza sauti kwa nguvu zao zote, wakamusifu Yawe kwa sababu ya kuanza kujenga musingi wa nyumba ya Yawe.