Ezra 3:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wengi wa makuhani, Walawi, na viongozi wa koo waliokuwa wazee na ambao walikuwa wameiona nyumba ya kwanza, walilia kwa sauti kubwa walipouona msingi wa nyumba hii mpya unawekwa, ingawa watu wengine wengi walipaza sauti kwa furaha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini wengi wa makuhani wazee, Walawi na viongozi wa jamaa waliokuwa wameona Hekalu la mwanzoni, walilia kwa sauti walipoona msingi wa Hekalu hili ukiwekwa, huku wengine wengi wakipiga kelele kwa furaha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali makuhani wengi, na Walawi, na wakuu wa mbari za mababa, waliokuwa wameiona nyumba ya kwanza, wakati msingi wa nyumba hii ulipowekwa mbele ya macho yao, walilia kwa sauti kuu; na watu wengi walipiga kelele za furaha;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wengi wa makuhani, Walawi, na viongozi wa koo waliokuwa wazee na ambao walikuwa wameiona nyumba ya kwanza, walilia kwa sauti kubwa walipouona msingi wa nyumba hii mpya unawekwa, ingawa watu wengine wengi walipaza sauti kwa furaha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini wengi wa makuhani wazee, Walawi na viongozi wa jamaa ambao walikuwa wameona Hekalu la mwanzoni, walilia kwa sauti wakati walipoona msingi wa Hekalu hili ukiwekwa, huku wengine wengi wakipiga kelele kwa furaha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini wengi wa makuhani wazee, Walawi na viongozi wa jamaa waliokuwa wameona Hekalu la mwanzoni, walilia kwa sauti walipoona msingi wa Hekalu hili ukiwekwa, huku wengine wengi wakipiga kelele kwa furaha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bali makuhani wengi, na Walawi, na wakuu wa koo za mababa, waliokuwa wameiona nyumba ya kwanza, wakati msingi wa nyumba hii ulipowekwa mbele ya macho yao, walilia kwa sauti kuu; na watu wengi walipiga kelele za furaha;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wengi wa makuhani, Walawi, na viongozi wa koo waliokuwa wazee na ambao walikuwa wameiona nyumba ya kwanza, walilia kwa sauti kubwa walipouona msingi wa nyumba hii mpya unawekwa, ingawa watu wengine wengi walipaza sauti kwa furaha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wengi wao watambikaji na Walawi nao waliokuwa vichwa vya milango, ndio wazee walioiona Nyumba ya kwanza wakalia machozi kwa sauti kuu, misingi ya Nyumba hii ilipowekwa machoni pao, lakini wengine wengi wakazipaza sauti zao za kupiga shangwe na kelele za furaha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali makuhani wengi, na Walawi, na wakuu wa mbari za mababa, waliokuwa wameiona nyumba ya kwanza, wakati msingi wa nyumba hii ulipowekwa mbele ya macho yao, walilia kwa sauti kuu; na watu wengi walipiga kelele za furaha;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wengi kati ya makuhani, Walawi, na viongozi wa ukoo waliokuwa wazee na ambao walikuwa wameiona nyumba ya kwanza, wakalia kwa sauti kubwa walipouona musingi wa nyumba hii mupya unawekwa, ingawa watu wengine wengi walipaza sauti kwa furaha.