Ezra 3:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walitoa pia sadaka za kawaida ambazo ziliteketezwa nzima, sadaka zilizotolewa wakati wa sikukuu ya mwezi mpya na katika sikukuu nyingine zote alizoagiza Mwenyezi-Mungu. Pia, walitoa tambiko zote zilizotolewa kwa hiari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya hayo, walitoa sadaka za kuteketezwa za kawaida, sadaka za Mwezi Mwandamo na dhabihu zote za sikukuu takatifu za Mwenyezi Mungu zilizoamriwa, pamoja na zile sadaka za hiari zilizotolewa kwa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na baadaye sadaka ya kuteketezwa ya daima, na za mwandamo wa mwezi, na za sikukuu za Bwana, zilizoamriwa na kuwekwa wakfu, na za kila mtu aliyemtolea Bwana sadaka kwa hiari yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walitoa pia sadaka za kawaida ambazo ziliteketezwa nzima, sadaka zilizotolewa wakati wa sikukuu ya mwezi mpya na katika sikukuu nyingine zote alizoagiza Mwenyezi-Mungu. Pia, walitoa tambiko zote zilizotolewa kwa hiari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya hayo, walitoa sadaka za kuteketezwa za kawaida, sadaka za Mwezi Mwandamo na dhabihu zote za sikukuu takatifu za BWANA zilizoamuriwa, pamoja na zile sadaka za hiari zilizotolewa kwa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya hayo, walitoa sadaka za kuteketezwa za kawaida, sadaka za Mwezi Mwandamo na dhabihu zote za sikukuu takatifu za bwana zilizoamriwa, pamoja na zile sadaka za hiari zilizotolewa kwa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na baadaye sadaka ya kuteketezwa ya daima, na za mwandamo wa mwezi, na za sikukuu za BWANA, zilizoamriwa na kuwekwa wakfu, na za kila mtu aliyemtolea BWANA sadaka kwa hiari yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walitoa pia sadaka za kawaida ambazo ziliteketezwa nzima, sadaka zilizotolewa wakati wa sikukuu ya mwezi mpya na katika sikukuu nyingine zote alizoagiza Mwenyezi-Mungu. Pia, walitoa tambiko zote zilizotolewa kwa hiari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Baadaye makaitoa nayo ng'ombe ya tambiko isiyokoma kutolewa ya kila siku, nazo za miandamo ya mwezi, nazo za sikukuu zote za Bwana zilizowekwa kuwa takatifu, nazo za kila mtu aliyetaka mwenyewe kumtolea Bwana kipaji cha tambiko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na baadaye sadaka ya kuteketezwa ya daima, na za mwandamo wa mwezi, na za sikukuu za BWANA, zilizoamriwa na kuwekwa wakfu, na za kila mtu aliyemtolea BWANA sadaka kwa hiari yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walitoa vilevile sadaka za kawaida ambazo ziliteketezwa nzima, sadaka zilizotolewa wakati wa sikukuu ya mwandamo wa mwezi na katika sikukuu nyingine zote alizoagiza Yawe. Vilevile walitoa sadaka zote za mapenzi.