Ezra 3:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ingawa msingi wa hekalu la Mwenyezi-Mungu ulikuwa bado kuwekwa, watu walianza kutoa sadaka za kuteketezwa tangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ingawa bado msingi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu ulikuwa haujawekwa, watu walianza kutoa sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa Mwenyezi Mungu tangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba walianza kumtolea Bwana sadaka za kuteketezwa, lakini msingi wa hekalu la Bwana ulikuwa haujawekwa bado.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ingawa msingi wa hekalu la Mwenyezi-Mungu ulikuwa bado kuwekwa, watu walianza kutoa sadaka za kuteketezwa tangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ingawa bado msingi wa Hekalu la BWANA ulikuwa haujawekwa, watu walianza kutoa sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa BWANA tangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ingawa bado msingi wa Hekalu la bwana ulikuwa haujawekwa, watu walianza kutoa sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa bwana tangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba walianza kumtolea BWANA sadaka za kuteketezwa, lakini msingi wa hekalu la BWANA ulikuwa haujawekwa bado.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ingawa msingi wa hekalu la Mwenyezi-Mungu ulikuwa bado kuwekwa, watu walianza kutoa sadaka za kuteketezwa tangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ya kwanza ya mwezi wa saba ndiyo, waliyoanzia kumtolea Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, lakini Jumba la Bwana lilikuwa halijawekewa misingi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba walianza kumtolea BWANA sadaka za kuteketezwa, lakini msingi wa hekalu la BWANA ulikuwa haujawekwa bado.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ingawa musingi wa hekalu la Yawe ulikuwa bado kuwekwa, watu walianza kutoa sadaka za kuteketezwa kwa moto tangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba.