Ezra 3:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu walitoa fedha za kuwalipa maseremala na waashi, walitoa pia chakula, vinywaji na mafuta, ili vipelekwe katika miji ya Tiro na Sidoni kupata miti ya mierezi kutoka Lebanoni. Miti hiyo ililetwa kwa njia ya bahari hadi Yopa. Haya yote yalifanyika kwa msaada wa mfalme Koreshi wa Persia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha watu wakawapa mafundi wa uashi na useremala fedha, wakawapa watu wa Sidoni na Tiro vyakula, vinywaji na mafuta ili waweze kuleta magogo ya mwerezi kupitia bahari kutoka Lebanoni hadi Yafa, kama alivyoagiza Koreshi mfalme wa Uajemi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena waliwapa waashi na maseremala fedha; wakawapa watu wa Sidoni, na watu wa Tiro, chakula, na vinywaji, na mafuta, ili walete mierezi kutoka Lebanoni mpaka Yafa kwa njia ya bahari, kwa kadiri walivyopewa ruhusa na Koreshi, mfalme wa Uajemi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu walitoa fedha za kuwalipa maseremala na waashi, walitoa pia chakula, vinywaji na mafuta, ili vipelekwe katika miji ya Tiro na Sidoni kupata miti ya mierezi kutoka Lebanoni. Miti hiyo ililetwa kwa njia ya bahari hadi Yopa. Haya yote yalifanyika kwa msaada wa mfalme Koreshi wa Persia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha watu wakawapa mafundi wa uashi na useremala fedha, wakawapa watu wa Sidoni na Tiro vyakula, vinywaji na mafuta ili waweze kuleta magogo ya mierezi kwa njia ya bahari kutoka Lebanoni hadi Yafa, kama alivyoagiza Koreshi mfalme wa Uajemi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha watu wakawapa mafundi wa uashi na useremala fedha, wakawapa watu wa Sidoni na Tiro vyakula, vinywaji na mafuta ili waweze kuleta magogo ya mierezi kwa njia ya bahari kutoka Lebanoni hadi Yafa, kama alivyoagiza Koreshi mfalme wa Uajemi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena waliwapa waashi na maseremala fedha; wakawapa watu wa Sidoni, na watu wa Tiro, chakula, na vinywaji, na mafuta, ili walete mierezi kutoka Lebanoni mpaka Yafa kwa njia ya bahari, kwa kadiri walivyopewa ruhusa na Koreshi, mfalme wa Uajemi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu walitoa fedha za kuwalipa maseremala na waashi, walitoa pia chakula, vinywaji na mafuta, ili vipelekwe katika miji ya Tiro na Sidoni kupata miti ya mierezi kutoka Lebanoni. Miti hiyo ililetwa kwa njia ya bahari hadi Yopa. Haya yote yalifanyika kwa msaada wa mfalme Koreshi wa Persia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wakachanga fedha za kuwapa mafundi wa kuchonga mawe na miti, nao Wasidoni na Watiro wakawapa vilaji na vinywaji na mafuta, walete miti ya miangati toka kwao Libanoni wakiipitisha baharini hata Yafo, kwani Kiro, mfalme wa Wapersia, aliwapa ruhusa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena waliwapa waashi na maseremala fedha; wakawapa watu wa Sidoni, na watu wa Tiro, chakula, na vinywaji, na mafuta, ili walete mierezi kutoka Lebanoni mpaka Yafa kwa njia ya bahari, kwa kadiri walivyopewa ruhusa na Koreshi, mfalme wa Uajemi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu walitoa feza za kuwalipa waseremala na wajengaji, walitoa vilevile chakula, vinywaji na mafuta, kusudi vipelekwe katika miji ya Tiro na Sidona kubadilishwa na miti ya mierezi kutoka Lebanoni. Miti hiyo ililetwa kwa njia ya bahari mpaka Yopa. Haya yote yalifanyika kwa musaada wa mufalme Kiro wa Persia.