Ezra 4:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tungependa ufahamu, ewe mfalme, kuwa mji huu ukijengwa upya na kuta zake zikimalizika, watu hawatalipa kodi, ushuru wala ada, na hazina yako itapungua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zaidi ya hayo, yampasa mfalme ajue kwamba kama mji huu ukijengwa na kuta zake zikafanywa upya, hakutakuwa na ulipaji wa kodi wala ada au ushuru, hivyo hazina za mfalme zitaathirika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, ijulikane kwa mfalme, ya kuwa mji huu ukijengwa, na kuta zake zikimalizika, hawatatoa kodi, wala ada, wala ushuru, na mwisho wake wafalme watapata hasara.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tungependa ufahamu, ewe mfalme, kuwa mji huu ukijengwa upya na kuta zake zikimalizika, watu hawatalipa kodi, ushuru wala ada, na hazina yako itapungua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zaidi ya hayo, mfalme yampasa ajue kwamba kama mji huu ukijengwa na kuta zake zikafanywa upya, hakutakuwa na ulipaji wa kodi wala ada au ushuru, hivyo hazina ya kifalme itaathirika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zaidi ya hayo, mfalme yampasa ajue kwamba kama mji huu ukijengwa na kuta zake zikafanywa upya, hakutakuwa na ulipaji wa kodi wala ada au ushuru, hivyo hazina za mfalme zitaathirika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, ijulikane kwa mfalme, ya kuwa mji huu ukijengwa, na kuta zake zikimalizika, hawatatoa kodi, wala ada, wala ushuru, na mwisho wake wafalme watapata hasara.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tungependa ufahamu, ewe mfalme, kuwa mji huu ukijengwa upya na kuta zake zikimalizika, watu hawatalipa kodi, ushuru wala ada, na hazina yako itapungua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena na ijulike kwa mfalme, ya kuwa mji huu ukijengwa, boma lake likimalizwa, watu wake hawatatoa kodi wala ushuru wa forodhani wala wa njiani, mwisho wafalme watapungukiwa fedha zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, ijulikane kwa mfalme, ya kuwa mji huu ukijengwa, na kuta zake zikimalizika, hawatatoa kodi, wala ada, wala ushuru, na mwisho wake wafalme watapata hasara.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tungependa ufahamu, ewe mufalme, kwamba muji huu ukijengwa upya na kuta zake zikimalizika, watu hawatalipa kodi, malipo ya kuvuka mipaka, na mengine mbalimbali na hazina yako itapunguka.