Ezra 4:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
ili ufanye uchunguzi katika kumbukumbu za babu zako. Humo utagundua kwamba tangu zamani, mji huu ulikuwa mwasi na umewasumbua sana wafalme na watawala wa mikoa, na kuwa tangu zamani watu wake ni wachochezi sana; ndio sababu mji huo uliangamizwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ili ufanyike uchunguzi kwenye kumbukumbu ya maandishi ya waliokutangulia. Katika kumbukumbu hizi utagundua kwamba mji huu ni mwasi, unaowataabisha wafalme na majimbo, ni mahali pa maasi tangu zamani. Ndiyo maana mji huu uliharibiwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ili habari zitafutwe katika kitabu cha tarehe za baba zako; ndivyo utakavyopata kujua kwa kitabu cha tarehe ya kuwa mji huo ni mji mwasi, wenye kuwadhuru wafalme, na maliwali, na ya kuwa wenyeji wake wamefanya fitina katika mji huo zamani; ndiyo sababu mji huo ukaangamizwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
ili ufanye uchunguzi katika kumbukumbu za babu zako. Humo utagundua kwamba tangu zamani, mji huu ulikuwa mwasi na umewasumbua sana wafalme na watawala wa mikoa, na kuwa tangu zamani watu wake ni wachochezi sana; ndio sababu mji huo uliangamizwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ili kwamba ufanyike uchunguzi kwenye kumbukumbu ya maandishi ya waliokutangulia. Katika kumbukumbu hizi utagundua kwamba mji huu ni wa maasi, unaowataabisha wafalme na majimbo, ni mahali pa maasi tangu zamani. Ndiyo maana mji huu uliharibiwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ili kwamba ufanyike uchunguzi kwenye kumbukumbu ya maandishi ya waliokutangulia. Katika kumbukumbu hizi utagundua kwamba mji huu ni wa maasi, unaowataabisha wafalme na majimbo, ni mahali pa maasi tangu zamani. Ndiyo maana mji huu uliharibiwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ili habari zichunguzwe katika kitabu cha kumbukumbu za baba zako; ndivyo utakavyopata kujua kwa kitabu cha kumbukumbu ya kuwa mji huo ni mji mwasi, wenye kuwadhuru wafalme, na wakuu wa mikoa, na ya kuwa wenyeji wake wamefanya fitina katika mji huo zamani; ndiyo sababu mji huo ukaangamizwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
ili ufanye uchunguzi katika kumbukumbu za babu zako. Humo utagundua kwamba tangu zamani, mji huu ulikuwa mwasi na umewasumbua sana wafalme na watawala wa mikoa, na kuwa tangu zamani watu wake ni wachochezi sana; ndio sababu mji huo uliangamizwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa na wachunguze katika kitabu cha makumbusho ya baba zako. Ndipo, utakapoyaona humo kitabuni mwenye makumbusho, utajua, ya kuwa mji huu ni mji wenye ukatavu uliowaharibia wafalme nchi hata mali zao, hata mafujo wameyafanya kwao tangu siku za kale. Kwa sababu hii mji huo ukabomolewa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ili habari zitafutwe katika kitabu cha tarehe za baba zako; ndivyo utakavyopata kujua kwa kitabu cha tarehe ya kuwa mji huo ni mji mwasi, wenye kuwadhuru wafalme, na maliwali, na ya kuwa wenyeji wake wamefanya fitina katika mji huo zamani; ndiyo sababu mji huo ukaangamizwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kusudi ufanye uchunguzi katika kitabu cha habari za babu zako. Humo utagundua kwamba tangu zamani, muji huu ulikuwa wa waasi na umewasumbua sana wafalme na watawala wa majimbo, na kuwa tangu zamani watu wake ni wachochezi sana; ndiyo sababu muji huo uliangamizwa.