Ezra 4:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha mfalme akapeleka jibu lifuatalo: “Kwa mtawala Rehumu, kwa Shishai, katibu wa mkoa, pamoja na wenzenu wote wanaoishi Samaria na mahali penginepo katika mkoa wa magharibi ya Eufrate.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme alirudisha jibu hili: Kwa Rehumu, afisa msimamizi, mwandishi Shimshai na wenzenu wote wanaoishi katika Samaria na penginepo Ng’ambo ya Mto Frati: Salamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo mfalme akapeleka majibu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha mfalme akapeleka jibu lifuatalo: “Kwa mtawala Rehumu, kwa Shishai, katibu wa mkoa, pamoja na wenzenu wote wanaoishi Samaria na mahali penginepo katika mkoa wa magharibi ya Eufrate.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme alirudisha jibu hili: Kwa Rehumu, afisa msimamizi, mwandishi Shimshai na wenzenu wote wanaoishi katika Samaria na penginepo Ng'ambo ya Mto Eufrati: Salaam.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme alirudisha jibu hili: Kwa Rehumu, afisa msimamizi, mwandishi Shimshai na wenzenu wote wanaoishi katika Samaria na penginepo Ng’ambo ya Mto Frati: Salamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo mfalme akatuma majibu; Kwa Rehumu, mtawala, na Shimshai, mwandishi, na wenzao wengine waliokaa katika Samaria, na penginepo ng'ambo ya Mto, Salamu; na kadhalika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha mfalme akapeleka jibu lifuatalo: “Kwa mtawala Rehumu, kwa Shishai, katibu wa mkoa, pamoja na wenzenu wote wanaoishi Samaria na mahali penginepo katika mkoa wa magharibi ya Eufrate.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mfalme alipotuma jibu kwa mwenye amri Rehumu na kwa mwandishi Simusai na kwa wenzao wengine waliokaa Samaria na penginepo ng'ambo ya huko ya jito kubwa kwamba: Salamu na mengine yafuatayo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo mfalme akapeleka majibu; Kwa Rehumu, Bwana shauri, na Shimshai, mwandishi, na wenzao wengine waliokaa katika Samaria, na penginepo ng’ambo ya Mto, Salamu; wakadhalika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha mufalme akatuma jibu hili: Kwa mutawala Rehumu, kwa Simusayi, karani wa jimbo, pamoja na wenzenu wote wanaoishi Samaria na pahali pengine katika jimbo la upande wa magaribi wa muto Furati.