Ezra 4:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
walimwendea Zerubabeli na viongozi wa koo, na kumwambia, “Tafadhali tushirikiane katika ujenzi wa hekalu. Sisi kama nyinyi tunamwabudu Mungu wenu, na tumekuwa tukimtolea tambiko tangu zamani za Esar-hadoni, mfalme wa Ashuru aliyetuleta hapa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wakamjia Zerubabeli na viongozi wa jamaa, nao wakasema, “Turuhusuni tuwasaidie kujenga, kwa sababu sisi tunamtafuta Mungu wenu kama ninyi na tumekuwa tukimtolea dhabihu tangu wakati wa Esar-Hadoni mfalme wa Ashuru, aliyetuleta hapa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakamkaribia Zerubabeli, na wakuu wa mbari za mababa, wakawaambia, Na tujenge sisi nasi pamoja nanyi; kwa maana tunamtafuta Mungu wenu kama ninyi, nasi twamtolea dhabihu tangu zamani za Esar-hadoni, mfalme wa Ashuru, aliyetupandisha mpaka hapa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
walimwendea Zerubabeli na viongozi wa koo, na kumwambia, “Tafadhali tushirikiane katika ujenzi wa hekalu. Sisi kama nyinyi tunamwabudu Mungu wenu, na tumekuwa tukimtolea tambiko tangu zamani za Esar-hadoni, mfalme wa Ashuru aliyetuleta hapa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wakamjia Zerubabeli na viongozi wa jamaa, nao wakasema, “Turuhusuni tuwasaidie kujenga, kwa sababu sisi tunamtafuta Mungu wenu kama ninyi na tumekuwa tukimtolea dhabihu tangu wakati wa Esar-hadoni mfalme wa Ashuru, aliyetuleta hapa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wakamjia Zerubabeli na viongozi wa jamaa, nao wakasema, “Turuhusuni tuwasaidie kujenga, kwa sababu sisi tunamtafuta Mungu wenu kama ninyi na tumekuwa tukimtolea dhabihu tangu wakati wa Esar-Hadoni mfalme wa Ashuru, aliyetuleta hapa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakamkaribia Zerubabeli, na wakuu wa koo za mababa, wakawaambia, Na tujenge sisi nasi pamoja nanyi; kwa maana tunamtafuta Mungu wenu kama ninyi, nasi tumemtolea dhabihu tangu zamani za Esar-hadoni, mfalme wa Ashuru, aliyetupandisha mpaka hapa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
walimwendea Zerubabeli na viongozi wa koo, na kumwambia, “Tafadhali tushirikiane katika ujenzi wa hekalu. Sisi kama nyinyi tunamwabudu Mungu wenu, na tumekuwa tukimtolea tambiko tangu zamani za Esar-hadoni, mfalme wa Ashuru aliyetuleta hapa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, walipomkaribia Zerubabeli nao waliokuwa vichwa vya milango, wakawaambia: Na tujenge pamoja nanyi! Kwani nasi tunamtumikia Mungu wenu kama ninyi, tunamtambikia tangu hapo, Esari-Hadoni, mfalme wa Asuri, alipotuleta huku, tukae.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakamkaribia Zerubabeli, na wakuu wa mbari za mababa, wakawaambia, Na tujenge sisi nasi pamoja nanyi; kwa maana tunamtafuta Mungu wenu kama ninyi, nasi twamtolea dhabihu tangu zamani za Esar-hadoni, mfalme wa Ashuru, aliyetupandisha mpaka hapa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
wakamwendea Zerubabeli na viongozi wa ukoo, na kumwambia: “Tafazali tushirikiane katika ujenzi wa hekalu. Sisi kama vile ninyi tunamwabudu Mungu wenu, na tumekuwa tukimutolea sadaka tangu zamani za Esari-Hadoni, mufalme wa Asuria aliyetuleta hapa.”