Ezra 4:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara tu waliposomewa barua hii kutoka kwa Artashasta, Rehumu, katibu Shimshai na wenzao waliharakisha kwenda Yerusalemu na kuwalazimisha kwa nguvu Wayahudi waache kuujenga mji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara waliposomewa nakala ya barua ya Mfalme Artashasta, Rehumu na Shimshai aliyekuwa mwandishi na wenzao, walienda mara moja kwa Wayahudi huko Yerusalemu na kuwalazimisha kwa nguvu kusimamisha ujenzi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata nakala ya waraka huo wa mfalme Artashasta uliposomwa mbele ya Rehumu, Bwana shauri, na Shimshai, mwandishi, na wenzao, wakaenda Yerusalemu upesi, kwa Wayahudi, wakawakomesha kwa nguvu na kwa kuwashurutisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara tu waliposomewa barua hii kutoka kwa Artashasta, Rehumu, katibu Shimshai na wenzao waliharakisha kwenda Yerusalemu na kuwalazimisha kwa nguvu Wayahudi waache kuujenga mji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara waliposomewa nakala ya barua ya Mfalme Artashasta, Rehumu na Shimshai aliyekuwa mwandishi na wenzao, walikwenda mara moja kwa Wayahudi huko Yerusalemu na kuwalazimisha kwa nguvu kusimamisha ujenzi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara waliposomewa nakala ya barua ya Mfalme Artashasta, Rehumu na Shimshai aliyekuwa mwandishi na wenzao, walikwenda mara moja kwa Wayahudi huko Yerusalemu na kuwalazimisha kwa nguvu kusimamisha ujenzi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha nakala ya barua hiyo ya mfalme Artashasta iliposomwa mbele ya Rehumu, mtawala na Shimshai, mwandishi, na wenzao, wakaenda Yerusalemu upesi, kwa Wayahudi, wakawakomesha kwa nguvu na kwa kuwashurutisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara tu waliposomewa barua hii kutoka kwa Artashasta, Rehumu, katibu Shimshai na wenzao waliharakisha kwenda Yerusalemu na kuwalazimisha kwa nguvu Wayahudi waache kuujenga mji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Papo hapo mwandiko wa pili wa barua ya mfalme Artasasta uliposomwa masikioni pao Rehumu na mwandishi Simusai na wenzao, ndipo, walipopiga mbio kwenda Yerusalemu kwa wayuda, wakawakataza majengo kwa ukorofi na nguvu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata nakala ya waraka huo wa mfalme Artashasta uliposomwa mbele ya Rehumu, Bwana shauri, na Shimshai, mwandishi, na wenzao, wakaenda Yerusalemu upesi, kwa Wayahudi, wakawakomesha kwa nguvu na kwa kuwashurutisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mara tu waliposomewa barua hii kutoka kwa Artasasta, Rehumu, karani Simusayi na wenzao wakaharakisha kwenda Yerusalema na kuwalazimisha kwa nguvu Wayuda waache kuujenga muji.