Ezra 4:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena wakati wa utawala wa Artashasta, mfalme wa Persia, Bishlamu, Mithredathi, Tabeeli na rafiki zao, walimwandikia barua mfalme Artashasta. Barua hiyo iliandikwa kwa herufi za Kiaramu na kutafsiriwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia katika siku za utawala wa Artashasta mfalme wa Uajemi, Bishlamu, Mithredathi, Tabeeli pamoja na wenzao waliandika barua kwa Artashasta. Barua hiyo iliandikwa kwa mwandiko wa Kiaramu na katika lugha ya Kiaramu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tena, katika siku za Artashasta, Mithredathi, na Tabeeli na mabaki ya wenziwe, wakimwandikia Artashasta, mfalme wa Uajemi, salamu za heri; na mwandiko wa waraka huo, ukaandikwa kwa herufi za Kiaramu, na kunenwa kwa lugha ya Kiaramu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena wakati wa utawala wa Artashasta, mfalme wa Persia, Bishlamu, Mithredathi, Tabeeli na rafiki zao, walimwandikia barua mfalme Artashasta. Barua hiyo iliandikwa kwa herufi za Kiaramu na kutafsiriwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia katika siku za utawala wa Artashasta mfalme wa Uajemi, Bishlamu, Mithredathi, Tabeeli pamoja na wenzao waliandika barua kwa Artashasta. Barua hiyo iliandikwa kwa mwandiko wa Kiaramu na katika lugha ya Kiaramu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia katika siku za utawala wa Artashasta mfalme wa Uajemi, Bishlamu, Mithredathi, Tabeeli pamoja na wenzao waliandika barua kwa Artashasta. Barua hiyo iliandikwa kwa mwandiko wa Kiaramu na katika lugha ya Kiaramu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tena, katika siku za Artashasta, Mithredathi, na Tabeeli na wenzao wengine, wakimwandikia Artashasta, mfalme wa Uajemi, salamu za heri; na mwandiko wa waraka huo, ukaandikwa kwa herufi za Kiaramu, na kusomwa kwa lugha ya Kiaramu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena wakati wa utawala wa Artashasta, mfalme wa Persia, Bishlamu, Mithredathi, Tabeeli na rafiki zao, walimwandikia barua mfalme Artashasta. Barua hiyo iliandikwa kwa herufi za Kiaramu na kutafsiriwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku za Artasasta Bisilamu na Mitiridati na Tabeli na wenziwe wengine wakaandika barua kwa Artasasta, mfalme wa Wapersia; nayo maandiko ya barua hii yalikuwa yameandikwa Kishami, nayo maneno yake yalikuwa yamegeuzwa kuwa ya Kishami vilevile:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tena, katika siku za Artashasta, Mithredathi, na Tabeeli na mabaki ya wenziwe, wakimwandikia Artashasta, mfalme wa Uajemi, salamu za heri; na mwandiko wa waraka huo, ukaandikwa kwa herufi za Kiaramu, na kunenwa kwa lugha ya Kiaramu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena wakati wa utawala wa Artasasta, mufalme wa Persia, Bisilamu, Mitiredati, Tabeli na warafiki zao, wakamwandikia barua mufalme Artasasta. Barua hiyo iliandikwa katika herufi za Kiaramea na kutafsiriwa.