Ezra 5:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, ukipenda ewe mfalme, amuru uchunguzi ufanywe katika kumbukumbu za kifalme mjini Babuloni kama mfalme Koreshi alitoa amri nyumba hii ya Mungu ijengwe upya mjini Yerusalemu. Kisha, tunakuomba utujulishe maoni yako kuhusu jambo hili.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa, ikimpendeza mfalme, uchunguzi na ufanyike katika kumbukumbu za maandishi ya ufalme mjini Babeli, kuona kama kweli Mfalme Koreshi alitoa amri ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika Yerusalemu. Kisha tunaomba mfalme na atutumie uamuzi wake kuhusu jambo hili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, sasa, mfalme akiona vema, watu na watafute katika nyumba ya hazina ya mfalme, iliyoko huko Babeli, kama ni kweli ya kuwa mfalme Koreshi alitoa amri kuijenga nyumba hiyo ya Mungu katika Yerusalemu, na mfalme akatuletee habari ya mapenzi yake katika jambo hili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, ukipenda ewe mfalme, amuru uchunguzi ufanywe katika kumbukumbu za kifalme mjini Babuloni kama mfalme Koreshi alitoa amri nyumba hii ya Mungu ijengwe upya mjini Yerusalemu. Kisha, tunakuomba utujulishe maoni yako kuhusu jambo hili.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa kama ikimpendeza mfalme, uchunguzi na ufanyike katika kumbukumbu ya maandishi ya kifalme mjini Babeli kuona kama kweli Mfalme Koreshi alitoa amri ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika Yerusalemu. Kisha tunaomba mfalme na atutumie uamuzi wake kuhusu jambo hili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa kama ikimpendeza mfalme, uchunguzi na ufanyike katika kumbukumbu za maandishi ya ufalme mjini Babeli, kuona kama kweli Mfalme Koreshi alitoa amri ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika Yerusalemu. Kisha tunaomba mfalme na atutumie uamuzi wake kuhusu jambo hili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, sasa, mfalme akiona vema, watu na wachunguze katika nyumba ya hazina ya mfalme, iliyoko huko Babeli, kama ni kweli ya kuwa mfalme Koreshi alitoa amri kuijenga nyumba hiyo ya Mungu katika Yerusalemu, na mfalme akatutumie habari ya mapenzi yake kuhusu jambo hili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, ukipenda ewe mfalme, amuru uchunguzi ufanywe katika kumbukumbu za kifalme mjini Babuloni kama mfalme Koreshi alitoa amri nyumba hii ya Mungu ijengwe upya mjini Yerusalemu. Kisha, tunakuomba utujulishe maoni yako kuhusu jambo hili.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa vikiwa vyema kwake mfalme, na wachunguze nyumbani mwa vilimbiko vya mfalme huko Babeli, kama ni kweli, ya kuwa mfalme Kiro aliagiza kuijenga Nyumba hii ya Mungu humu Yerusalemu. Kisha mfalme na atume kwetu jibu la kutuambia ayatakayo, yafanyike katika jambo hili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, sasa, mfalme akiona vema, watu na watafute katika nyumba ya hazina ya mfalme, iliyoko huko Babeli, kama ni kweli ya kuwa mfalme Koreshi alitoa amri kuijenga nyumba hiyo ya Mungu katika Yerusalemu, na mfalme akatuletee habari ya mapenzi yake katika jambo hili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, ikikupendeza, ewe mufalme, amuru uchunguzi ufanyike katika kitabu cha habari za kifalme katika muji wa Bebeli kama mufalme Kiro alitoa amri nyumba hii ya Mungu ijengwe upya katika Yerusalema. Kisha, tunakuomba utujulishe maoni yako juu ya jambo hili.