Ezra 5:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Tatenai, mtawala wa mkoa wa magharibi ya Eufrate, Shethar-bozenai na wenzao, wakamwandikia mfalme Dario.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hii ni nakala ya barua ile Tatenai, mtawala wa ng’ambo ya mto Frati na Shethar-Bozenai na wenzao maafisa wa ng’ambo ya mto Frati waliyompelekea Mfalme Dario.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hii ndiyo nakala ya waraka waliyompelekea mfalme Dario; na Tatenai, liwali wa ng'ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzake wa Kiajemi, waliokuwako huko ng'ambo ya Mto,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Tatenai, mtawala wa mkoa wa magharibi ya Eufrate, Shethar-bozenai na wenzao, wakamwandikia mfalme Dario.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hii ni nakala ya barua ile Tatenai, mtawala wa ng'ambo ya mto Eufrati na Shethar-Bozenai na wenzao maafisa wa ng'ambo ya mto Eufrati waliyompelekea Mfalme Dario.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hii ni nakala ya barua ile Tatenai, mtawala wa ng’ambo ya mto Frati na Shethar-Bozenai na wenzao maafisa wa ng’ambo ya mto Frati waliyompelekea Mfalme Dario.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hii ndiyo nakala ya waraka ambao; Tatenai, Mkuu wa mkoa wa ng'ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzake wa Kiajemi, waliokuwako huko ng'ambo ya Mto; walimtumia mfalme Dario.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Tatenai, mtawala wa mkoa wa magharibi ya Eufrate, Shethar-bozenai na wenzao, wakamwandikia mfalme Dario.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwandiko wa pili wa barua, waliyoituma kwa mfalme Dario akina Tatinai, mtawala nchi zilizoko upande wa huku wa jito kubwa, na Setari-Bozinai na wenzake Waafarsaki waliokaa upande wa huku wa jito kubwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hii ndiyo nakala ya waraka waliyompelekea mfalme Dario; na Tatenai, liwali wa ng’ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzake wa Kiajemi, waliokuwako huko ng’ambo ya Mto,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Tatenayi, mutawala wa jimbo la upande wa magaribi wa muto Furati, Setari-Bozenayi na wenzao, wakamwandikia mufalme Dario.