Ezra 6:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Dario alitoa amri na uchunguzi ulifanywa mjini Babuloni katika nyumba ya kumbukumbu za kifalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Mfalme Dario alitoa amri, nao wakafanya uchunguzi katika kumbukumbu zilizohifadhiwa katika hazina huko Babeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo mfalme Dario akatoa amri, na watu wakatafuta katika nyumba ya vyuo vya tarehe, hapo akiba zilipowekwa katika Babeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Dario alitoa amri na uchunguzi ulifanywa mjini Babuloni katika nyumba ya kumbukumbu za kifalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Mfalme Dario alitoa amri, nao wakafanya uchunguzi katika kumbukumbu zilizohifadhiwa katika hazina huko Babeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Mfalme Dario alitoa amri, nao wakafanya uchunguzi katika kumbukumbu zilizohifadhiwa katika hazina huko Babeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo mfalme Dario akatoa amri, na watu wakachunguza katika nyumba ya kuhifadhia vitabu vya kumbukumbu ambapo hati ziliwekwa katika Babeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Dario alitoa amri na uchunguzi ulifanywa mjini Babuloni katika nyumba ya kumbukumbu za kifalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mfalme Dario alipotoa amri, wakachunguza nyumbani mwenye vitabu, mlimowekwa navyo vilimbiko vya huko Babeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo mfalme Dario akatoa amri, na watu wakatafuta katika nyumba ya vyuo vya tarehe, hapo akiba zilipowekwa katika Babeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Dario alitoa amri na uchunguzi ukafanywa katika muji wa Babeli katika nyumba ya kuwekea maandiko ya zamani ya kifalme.