Ezra 6:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naamuru pia kwamba mtu yeyote ambaye hatatii amri hii, boriti ingolewe kutoka katika nyumba yake, na atumbuliwe kwayo. Tena, nyumba yake na ifanywe kuwa rundo la mavi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zaidi ya hayo, ninaamuru kwamba mtu yeyote atakayebadilisha amri hii, boriti itang’olewa kutoka nyumba yake, ichongwe upande mmoja na atumbuliwe nayo. Kwa ajili ya kosa hili nyumba yake ifanywe lundo la taka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Pia nimetoa amri kwamba, mtu awaye yote atakayelibadili neno hili, boriti na itolewe katika nyumba yake, akainuliwe na kutungikwa juu yake; tena nyumba yake ikafanywe jaa kwa ajili ya neno hili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naamuru pia kwamba mtu yeyote ambaye hatatii amri hii, boriti ing'olewe kutoka katika nyumba yake, na atumbuliwe kwayo. Tena, nyumba yake na ifanywe kuwa rundo la mavi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zaidi ya hayo, ninaamuru kwamba mtu ye yote atakayebadilisha amri hii, boriti itang'olewa kutoka katika nyumba yake, ichongwe upande mmoja na atumbuliwe nayo. Kwa ajili ya kosa hili nyumba yake ifanywe lundo la taka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zaidi ya hayo, ninaamuru kwamba mtu yeyote atakayebadilisha amri hii, boriti itang’olewa kutoka nyumba yake, ichongwe upande mmoja na atumbuliwe nayo. Kwa ajili ya kosa hili nyumba yake ifanywe lundo la taka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Pia nimetoa amri kwamba, mtu awaye yote atakayelibadili neno hili, boriti na itolewe katika nyumba yake, akainuliwe na kutungikwa juu yake; tena nyumba yake ikafanywe jaa kwa ajili ya neno hili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naamuru pia kwamba mtu yeyote ambaye hatatii amri hii, boriti ingolewe kutoka katika nyumba yake, na atumbuliwe kwayo. Tena, nyumba yake na ifanywe kuwa rundo la mavi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena ninatoa amri kwamba: Kila mtu atakayeligeuza neno hili nyumbani mwake itolewe nguzo, isimikwe, kisha mwenyewe atundikwe humo, nayo nyumba yake igeuzwe kuwa kifusi kwa ajili hiyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Pia nimetoa amri kwamba, mtu awaye yote atakayelibadili neno hili, boriti na itolewe katika nyumba yake, akainuliwe na kutungikwa juu yake; tena nyumba yake ikafanywe jaa kwa ajili ya neno hili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninaamuru vilevile kwamba mutu yeyote ambaye hatatii amri hii, muti mumoja uongolewe kutoka katika nyumba yake na atundikwe juu yake. Tena, nyumba yake ifanywe kuwa yalala.