Ezra 6:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Tatenai, mtawala wa mkoa wa magharibi ya mto Eufrate, Shethar-bozenai, na maofisa wenzao, wakafanya bidii kutekeleza maagizo ya mfalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu ya amri aliyotoa Mfalme Dario, Tatenai mtawala wa Ng’ambo ya Mto Frati na Shethar-Bozenai na wenzao wakaitekeleza kwa bidii na kwa makini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Tatenai, liwali wa ng'ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzi wao, wakafanya hayo kwa bidii, kwa sababu mfalme Dario alikuwa ametuma watu kwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Tatenai, mtawala wa mkoa wa magharibi ya mto Eufrate, Shethar-bozenai, na maofisa wenzao, wakafanya bidii kutekeleza maagizo ya mfalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu ya amri aliyotoa Mfalme Dario, Tatenai mtawala wa Ng'ambo ya Mto Eufrati na Shethar-Bozenai na wenzao wakaitekeleza kwa bidii na kwa makini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu ya amri aliyotoa Mfalme Dario, Tatenai mtawala wa Ng’ambo ya Mto Frati na Shethar-Bozenai na wenzao wakaitekeleza kwa bidii na kwa makini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Tatenai, mtawala wa ng'ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzao, wakafanya hayo kwa bidii, kwa sababu mfalme Dario alikuwa ametuma watu kwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Tatenai, mtawala wa mkoa wa magharibi ya mto Eufrate, Shethar-bozenai, na maofisa wenzao, wakafanya bidii kutekeleza maagizo ya mfalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo Tatinai, mtawala nchi zilizoko ng'ambo ya huku ya jito kubwa, na Setari-Bozinai na wenzao wakafanya sawasawa kabisa, kama mfalme Dario alivyowaagiza katika hiyo barua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Tatenai, liwali wa ng’ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzi wao, wakafanya hayo kwa bidii, kwa sababu mfalme Dario alikuwa ametuma watu kwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Tatenayi, mutawala wa jimbo la upande wa magaribi wa muto Furati, Setari-Bozenayi, na wakubwa wenzao, wakafanya bidii kwa kutimiza maagizo ya mufalme.