Ezra 6:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Pia, kwa ajili ya huduma ya Mungu katika Yerusalemu, waliwapanga makuhani katika makundi yao ya Walawi katika zamu zao kufuatana na maagizo yaliyoandikwa katika kitabu cha Mose.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakawaweka makuhani katika nafasi zao na Walawi wakawekwa katika makundi yao ya huduma kwa Mungu huko Yerusalemu, kulingana na ilivyoandikwa katika Kitabu cha Musa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakawaweka makuhani katika kura zao, wakawaweka na Walawi katika zamu zao, kwa ajili ya huduma ya Mungu, iliyokuwako Yerusalemu; vile vile kama vilivyoandikwa katika chuo cha Musa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Pia, kwa ajili ya huduma ya Mungu katika Yerusalemu, waliwapanga makuhani katika makundi yao ya Walawi katika zamu zao kufuatana na maagizo yaliyoandikwa katika kitabu cha Mose.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakawaweka makuhani katika nafasi zao na Walawi wakawekwa katika makundi yao ya huduma kwa Mungu huko Yerusalemu, kulingana na ilivyoandikwa katika Kitabu cha Mose.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakawaweka makuhani katika nafasi zao na Walawi wakawekwa katika makundi yao ya huduma kwa Mungu huko Yerusalemu, kulingana na ilivyoandikwa katika Kitabu cha Musa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakawaweka makuhani katika sehemu zao, wakawaweka na Walawi katika zamu zao, kwa ajili ya huduma ya Mungu, iliyokuwako Yerusalemu; kama ilivyoandikwa katika chuo cha Musa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Pia, kwa ajili ya huduma ya Mungu katika Yerusalemu, waliwapanga makuhani katika makundi yao ya Walawi katika zamu zao kufuatana na maagizo yaliyoandikwa katika kitabu cha Mose.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wakaweka watambikaji kwa vyama vyao nao Walawi kwa kura zao, walizopigiwa, wamtumikie Mungu mle Yerusalemu, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Mose.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakawaweka makuhani katika kura zao, wakawaweka na Walawi katika zamu zao, kwa ajili ya huduma ya Mungu, iliyokuwako Yerusalemu; vile vile kama vilivyoandikwa katika chuo cha Musa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile, kwa ajili ya kazi ya Mungu katika Yerusalema, waliwapanga makuhani katika makundi yao ya Walawi katika zamu zao kufuatana na maagizo yaliyoandikiwa katika kitabu cha Musa.