Ezra 6:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waliokula mwanakondoo wa Pasaka walikuwa Waisraeli wote waliorudi kutoka uhamishoni pamoja na watu wengine wote ambao walikuwa wameziacha njia za mataifa mengine ili kumwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Waisraeli waliorudi kutoka uhamishoni wakala Pasaka, pamoja na wale waliokuwa wamejitenga na matendo ya unajisi wa Mataifa jirani ili kumtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wana wa Israeli wakaila, wale waliorudi kuitoka nchi ya uhamisho wao, na watu wote ambao pamoja nao wamejitenga na uchafu wa taifa za nchi, ili kumtaka Bwana, Mungu wa Israeli,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waliokula mwanakondoo wa Pasaka walikuwa Waisraeli wote waliorudi kutoka uhamishoni pamoja na watu wengine wote ambao walikuwa wameziacha njia za mataifa mengine ili kumwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Waisraeli waliokuwa wamerudi kutoka utumwani uhamishoni wakaila Pasaka, pamoja na wale waliokuwa wamejitenga na matendo ya unajisi wa Mataifa ya jirani ili kumtafuta BWANA, Mungu wa Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Waisraeli waliokuwa wamerudi kutoka utumwani uhamishoni wakaila Pasaka, pamoja na wale waliokuwa wamejitenga na matendo ya unajisi wa Mataifa ya jirani ili kumtafuta bwana, Mungu wa Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wana wa Israeli wakaila, wale waliorudi kutoka nchi ya uhamisho wao, na watu wote ambao pamoja nao wamejitenga na uchafu wa taifa za nchi, ili kumtaka BWANA, Mungu wa Israeli,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waliokula mwanakondoo wa Pasaka walikuwa Waisraeli wote waliorudi kutoka uhamishoni pamoja na watu wengine wote ambao walikuwa wameziacha njia za mataifa mengine ili kumwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa Isiraeli waliorudi kwenye kutekwa wakaila pamoja nao waliotaka kumfuata Bwana Mungu wa Isiraeli, waliojitenga, wasijichafue kwa wamizimu wenzao waliokaa kwao katika nchi hii.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wana wa Israeli wakaila, wale waliorudi kuitoka nchi ya uhamisho wao, na watu wote ambao pamoja nao wamejitenga na uchafu wa taifa za nchi, ili kumtaka BWANA, Mungu wa Israeli,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waliokula mwana-kondoo wa Pasaka walikuwa Waisraeli wote waliorudi kutoka katika uhamisho pamoja na watu wengine wote ambao walikuwa wameziacha njia za mataifa mengine kwa kumwabudu Yawe, Mungu wa Israeli.