Ezra 6:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mnamo mwaka wa kwanza wa utawala wake, mfalme Koreshi alitoa amri nyumba ya Mungu ijengwe upya mjini Yerusalemu, na iwe mahali pa kutolea tambiko na sadaka za kuteketezwa. Kimo chake kitakuwa mita 27 na upana wake mita 27.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Mfalme Koreshi, mfalme alitoa amri kuhusu Hekalu la Mungu katika Yerusalemu: Hekalu na lijengwe upya likiwa mahali pa kutolea dhabihu, na misingi yake ijengwe. Iwe na kimo cha mikono sitini, upana wa mikono sitini,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika mwaka wa kwanza wa mfalme Koreshi, mfalme Koreshi alitoa amri, Kwa habari ya nyumba ya Mungu huko Yerusalemu, nyumba hiyo na ijengwe, mahali watoapo dhabihu, na misingi yake ipigwe na kufanywa imara sana; kuinuka kwake kuwe mikono sitini, na upana wake mikono sitini;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mnamo mwaka wa kwanza wa utawala wake, mfalme Koreshi alitoa amri nyumba ya Mungu ijengwe upya mjini Yerusalemu, na iwe mahali pa kutolea tambiko na sadaka za kuteketezwa. Kimo chake kitakuwa mita 27 na upana wake mita 27.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mwaka wa kwanza wa kutawala Mfalme Koreshi, mfalme alitoa amri kuhusu Hekalu la Mungu katika Yerusalemu: Hekalu na lijengwe tena mahali pale pale Wayahudi walipokuwa wakitoa dhabihu, kwenye msingi ule ule. Iwe na kimo cha mikono sitini, upana wa mikono sitini,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mwaka wa kwanza wa kutawala Mfalme Koreshi, mfalme alitoa amri kuhusu Hekalu la Mungu katika Yerusalemu: Hekalu na lijengwe tena mahali palepale Wayahudi walipokuwa wakitoa dhabihu, kwenye msingi ule ule. Iwe na kimo cha mikono sitini, upana wa mikono sitini,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika mwaka wa kwanza wa mfalme Koreshi, mfalme Koreshi alitoa amri, Kuhusu nyumba ya Mungu huko Yerusalemu, nyumba hiyo na ijengwe, mahali watoapo dhabihu, na misingi yake ipigwe na kufanywa imara sana; kuinuka kwake kuwe mikono sitini, na upana wake mikono sitini;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mnamo mwaka wa kwanza wa utawala wake, mfalme Koreshi alitoa amri nyumba ya Mungu ijengwe upya mjini Yerusalemu, na iwe mahali pa kutolea tambiko na sadaka za kuteketezwa. Kimo chake kitakuwa mita 27 na upana wake mita 27.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwamba: Katika mwaka wa kwanza wa mfalme Kiro huyu mfalme Kiro akatoa amri, Nyumba ya Mungu huko Yerusalemu na ijengwe kuwa mahali, watakapotoa ng'ombe za tambiko, misingi yake itengenezwe kuwa na nguvu; urefu wake uwe mikono sitini, nao upana wake uwe mikono sitini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika mwaka wa kwanza wa mfalme Koreshi, mfalme Koreshi alitoa amri, Kwa habari ya nyumba ya Mungu huko Yerusalemu, nyumba hiyo na ijengwe, mahali watoapo dhabihu, na misingi yake ipigwe na kufanywa imara sana; kuinuka kwake kuwe mikono sitini, na upana wake mikono sitini;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Katika mwaka wa kwanza wa utawala wake, mufalme Kiro alitoa amri kwamba nyumba ya Mungu ijengwe upya katika Yerusalema, na ikuwe pahali pa kutolea sadaka na sadaka za kuteketezwa kwa moto. Urefu wake kwenda juu utakuwa metre makumi mbili na saba na upana wake metre makumi mbili na saba.