Ezra 6:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Zaidi ya hayo, natoa amri kwamba nyinyi mtawasaidia katika kazi hiyo. Gharama zao zote zitalipwa bila kuchelewa kutoka katika hazina ya mfalme inayotokana na kodi kutoka katika mkoa wa magharibi wa mto Eufrate.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zaidi ya hayo, hapa natoa amri kuhusu mtakalofanya kwa ajili ya wazee wa Wayahudi katika ujenzi wa nyumba hii ya Mungu: Gharama za watu hawa zitalipwa kikamilifu kutoka hazina ya mfalme, kutoka mapato ya Ng’ambo ya Mto Frati, ili ujenzi usisimame.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena, natoa amri kuwaagiza ninyi mtakayowatendea wazee hao wa Wayahudi, kwa kazi hii ya kuijenga nyumba ya Mungu; katika mali ya mfalme, yaani, katika kodi za nchi iliyo ng'ambo ya Mto, watu hao wapewe gharama zote kwa bidii, ili wasizuiliwe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Zaidi ya hayo, natoa amri kwamba nyinyi mtawasaidia katika kazi hiyo. Gharama zao zote zitalipwa bila kuchelewa kutoka katika hazina ya mfalme inayotokana na kodi kutoka katika mkoa wa magharibi wa mto Eufrate.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zaidi ya hayo, hapa natoa amri kuhusu mtakalofanya kwa ajili ya wazee wa Wayahudi katika ujenzi wa nyumba hii ya Mungu: Gharama za watu hawa zitalipwa kikamilifu kutoka katika hazina ya mfalme, kutoka kwenye mapato ya Ng'ambo ya Mto Eufrati, ili ujenzi usisimame.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zaidi ya hayo, hapa natoa amri kuhusu mtakalofanya kwa ajili ya wazee wa Wayahudi katika ujenzi wa nyumba hii ya Mungu: Gharama za watu hawa zitalipwa kikamilifu kutoka hazina ya mfalme, kutoka kwenye mapato ya Ng’ambo ya Mto Frati, ili ujenzi usisimame.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena, natoa amri kuwaagiza ninyi mtakayowatendea wazee hao wa Wayahudi, kwa kazi hii ya kuijenga nyumba ya Mungu; kwa mali ya mfalme, yaani, kwa kodi za nchi iliyo ng'ambo ya Mto, watu hao wapewe gharama zote bila kukawia, ili wasizuiliwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Zaidi ya hayo, natoa amri kwamba nyinyi mtawasaidia katika kazi hiyo. Gharama zao zote zitalipwa bila kuchelewa kutoka katika hazina ya mfalme inayotokana na kodi kutoka katika mkoa wa magharibi wa mto Eufrate.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi natoa amri, ya kwamba msaidiane na hao wazee katika kuijenga Nyumba hiyo ya Mungu, mkifanya bidii, mpate kutoa mali za mfalme zitokazo katika kodi za nchi zilizoko ng'ambo ya huko ya jito kubwa, watu hao wapewe kila mara fedha za kuzilipa hizo hazi, wasizuiliwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena, natoa amri kuwaagiza ninyi mtakayowatendea wazee hao wa Wayahudi, kwa kazi hii ya kuijenga nyumba ya Mungu; katika mali ya mfalme, yaani, katika kodi za nchi iliyo ng’ambo ya Mto, watu hao wapewe gharama zote kwa bidii, ili wasizuiliwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zaidi ya hayo, ninatoa amri kwamba ninyi mutawasaidia katika kazi hiyo. Mali zao zote walizotumia zitalipwa bila kuchelewa kutoka katika hazina ya mufalme inayotokana na kodi kutoka katika jimbo la upande wa magaribi wa muto Furati.