Ezra 6:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila siku, tena bila kukosa, mtawapa makuhani wa Yerusalemu kila kitu watakachohitaji; iwe ni fahali wachanga, kondoo dume au wanakondoo wa sadaka za kuteketezwa kwa Mungu wa mbinguni, au ngano, chumvi, divai au mafuta.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Chochote kinachohitajika kama mafahali wachanga, kondoo dume, wana-kondoo kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa Mungu wa mbinguni, ngano, chumvi, divai na mafuta kama vitakavyohitajika na makuhani huko Yerusalemu, lazima wapewe kila siku pasipo kukosa,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kila kitu wanachokihitaji, katika ng'ombe wachanga, na kondoo waume, na wana-kondoo, kwa sadaka za kuteketezwa watakazomtolea Mungu wa mbinguni, na ngano, na chumvi, na divai, na mafuta, kama makuhani walioko Yerusalemu watakavyosema, na wapewe vitu hivyo vyote siku kwa siku, msikose kuwapa;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila siku, tena bila kukosa, mtawapa makuhani wa Yerusalemu kila kitu watakachohitaji; iwe ni fahali wachanga, kondoo dume au wanakondoo wa sadaka za kuteketezwa kwa Mungu wa mbinguni, au ngano, chumvi, divai au mafuta.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Cho chote kinachohitajika kama mafahali wachanga, kondoo waume, wana-kondoo kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa Mungu wa mbinguni, ngano, chumvi, divai na mafuta kama vitakavyohitajika na makuhani huko Yerusalemu, lazima wapewe kila siku pasipo kukosa,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Chochote kinachohitajika kama mafahali wachanga, kondoo dume, wana-kondoo kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa Mungu wa mbinguni, ngano, chumvi, divai na mafuta kama vitakavyohitajika na makuhani huko Yerusalemu, lazima wapewe kila siku pasipo kukosa,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kila kitu wanachokihitaji, katika ng'ombe wachanga, na kondoo dume, na wana-kondoo, kwa sadaka za kuteketezwa watakazomtolea Mungu wa mbinguni, na ngano, na chumvi, na divai, na mafuta, kama makuhani walioko Yerusalemu watakavyosema, na wapewe vitu hivyo vyote siku kwa siku, msikose kuwapa;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila siku, tena bila kukosa, mtawapa makuhani wa Yerusalemu kila kitu watakachohitaji; iwe ni fahali wachanga, kondoo dume au wanakondoo wa sadaka za kuteketezwa kwa Mungu wa mbinguni, au ngano, chumvi, divai au mafuta.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo mengine wanayopaswa nayo, kama madume ya ndama na madume ya kondoo na wana kondoo wa kuwa ng'ombe za tambiko za Mungu wa mbingu, tena ngano na chumvi na mvinyo na mafuta, kama watambikaji walioko Yerusalemu wanavyovitaka, sharti wapewe siku kwa siku, visikoseke,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kila kitu wanachokihitaji, katika ng’ombe wachanga, na kondoo waume, na wana-kondoo, kwa sadaka za kuteketezwa watakazomtolea Mungu wa mbinguni, na ngano, na chumvi, na divai, na mafuta, kama makuhani walioko Yerusalemu watakavyosema, na wapewe vitu hivyo vyote siku kwa siku, msikose kuwapa;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila siku, tena bila kukosa, mutawapa makuhani wa Yerusalema kila kitu watakachohitaji; ikuwe ni ngombe dume, wana-ngombe, kondoo dume au wana-kondoo wa sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa ajili ya Mungu wa mbinguni, au ngano, chumvi, divai au mafuta.