Ezra 7:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ezra alikuwa amejitoa kwa moyo wote kujifunza sheria ya Mwenyezi-Mungu, kuitii na kuwafundisha watu wa Israeli maagizo na amri zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana Ezra alikuwa amejitoa kwa moyo wote kujifunza na kushika Torati ya Mwenyezi Mungu na kuwafundisha Waisraeli amri na sheria zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana huyo Ezra alikuwa ameuelekeza moyo wake kuitafuta sheria ya Bwana, na kuitenda, na kufundisha maagizo na hukumu katika Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ezra alikuwa amejitoa kwa moyo wote kujifunza sheria ya Mwenyezi-Mungu, kuitii na kuwafundisha watu wa Israeli maagizo na amri zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana Ezra alikuwa amejitoa kwa moyo wote kujifunza na kushika sheria ya BWANA na kuwafundisha watu wa Israeli amri na sheria zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana Ezra alikuwa amejitoa kwa moyo wote kujifunza na kushika Torati ya bwana na kuwafundisha watu wa Israeli amri na sheria zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana huyo Ezra alikuwa ameuelekeza moyo wake kuitafuta sheria ya BWANA, na kuitenda, na kufundisha maagizo na hukumu katika Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ezra alikuwa amejitoa kwa moyo wote kujifunza sheria ya Mwenyezi-Mungu, kuitii na kuwafundisha watu wa Israeli maagizo na amri zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Ezera alikuwa ameuelekeza moyo wake kuyatafuta Maonyo ya Bwana, ayafanye, tena awafundishe Waisiraeli maongozi na maamuzi yapasayo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana huyo Ezra alikuwa ameuelekeza moyo wake kuitafuta sheria ya BWANA, na kuitenda, na kufundisha maagizo na hukumu katika Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ezra alikuwa amejitoa kwa moyo wote kujifunza Sheria ya Yawe, kuitii na kuwafundisha watu wa Israeli masharti na maagizo zake.