Ezra 7:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi mfalme Artashasta, natoa amri kwa waweka hazina wote katika mkoa wa magharibi ya mto Eufrate kwamba chochote atakachohitaji Ezra, kuhani na mwandishi wa sheria ya Mungu wa mbinguni, mtampa, tena bila kusita,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi, Mfalme Artashasta, sasa naagiza watunza hazina wote wa Ng’ambo ya Mto Frati kutoa kwa bidii chochote kwa Ezra kuhani na mwalimu wa Torati ya Mungu wa mbinguni atakachohitaji kwenu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mimi, naam mimi, mfalme Artashasta, nawapa amri wote wenye kutunza hazina, walio ng'ambo ya Mto, ya kwamba, kila neno ambalo Ezra, kuhani, mwandishi wa torati ya Mungu wa mbinguni, atalitaka kwenu, na litendeke kwa bidii nyingi,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi mfalme Artashasta, natoa amri kwa waweka hazina wote katika mkoa wa magharibi ya mto Eufrate kwamba chochote atakachohitaji Ezra, kuhani na mwandishi wa sheria ya Mungu wa mbinguni, mtampa, tena bila kusita,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi, Mfalme Artashasta, sasa naagiza watunza hazina wote wa Ng'ambo ya Mto Eufrati kutoa kwa bidii cho chote kwa Ezra kuhani na mwalimu wa Sheria ya Mungu wa mbinguni atakachohitaji kwenu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi, Mfalme Artashasta, sasa naagiza watunza hazina wote wa Ng’ambo ya Mto Frati kutoa kwa bidii chochote kwa Ezra kuhani na mwalimu wa Torati ya Mungu wa mbinguni atakachohitaji kwenu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mimi, naam mimi, mfalme Artashasta, nawapa amri watunza hazina wote, walio ng'ambo ya Mto, ya kwamba, kila neno ambalo Ezra, kuhani, mwandishi wa Torati ya Mungu wa mbinguni, atalitaka kwenu, na litendeke kwa bidii nyingi,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi mfalme Artashasta, natoa amri kwa waweka hazina wote katika mkoa wa magharibi ya mto Eufrate kwamba chochote atakachohitaji Ezra, kuhani na mwandishi wa sheria ya Mungu wa mbinguni, mtampa, tena bila kusita,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena mimi mfalme Artasasta ninawatolea amri watunza mali wote walioko ng'ambo ya huko ya jito kubwa kwamba: Yote, mtambikaji Ezera anayeyajua vema Maonyo ya Mungu wa mbingu atakayowaomba ninyi, yafanyike sawasawa,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mimi, naam mimi, mfalme Artashasta, nawapa amri wote wenye kutunza hazina, walio ng’ambo ya Mto, ya kwamba, kila neno ambalo Ezra, kuhani, mwandishi wa torati ya Mungu wa mbinguni, atalitaka kwenu, na litendeke kwa bidii nyingi,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi mufalme Artasasta, ninatoa amri kwa walinzi wa hazina wote katika jimbo la upande wa magaribi wa muto Furati kwamba kitu chochote Ezra atakachohitaji, kuhani na mwandishi wa Sheria ya Mungu wa mbinguni, mutamupa, tena bila kusita,