Ezra 7:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tunawafahamisheni pia kuwa ni marufuku kuwadai kodi ya mapato, ushuru au ada makuhani, Walawi, waimbaji, walinda mlango, wafanyakazi au watumishi wengine wa nyumba hii ya Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia ninyi fahamuni kuwa hamna mamlaka ya kuwatoza kodi, ushuru au ada makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, watumishi wa Hekalu au wafanyakazi wengine kwenye nyumba ya Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena twawaarifuni ya kuwa katika habari ya makuhani, na Walawi, na waimbaji, na mabawabu na Wanethini, au watumishi wa nyumba hii ya Mungu, si halali kuwatoza kodi, wala ada, wala ushuru.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tunawafahamisheni pia kuwa ni marufuku kuwadai kodi ya mapato, ushuru au ada makuhani, Walawi, waimbaji, walinda mlango, wafanyakazi au watumishi wengine wa nyumba hii ya Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia ninyi fahamuni kuwa hamna mamlaka ya kuwatoza kodi, ushuru au ada makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, Wanethini au wafanyakazi wengine kwenye nyumba ya Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia ninyi fahamuni kuwa hamna mamlaka ya kuwatoza kodi, ushuru au ada makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, watumishi wa Hekalu au wafanyakazi wengine kwenye nyumba ya Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena tunawaarifu ya kuwa katika habari ya makuhani, na Walawi, na waimbaji, na mabawabu na Wanethini, au watumishi wa nyumba hii ya Mungu, si halali kuwatoza kodi, wala ada, wala ushuru.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tunawafahamisheni pia kuwa ni marufuku kuwadai kodi ya mapato, ushuru au ada makuhani, Walawi, waimbaji, walinda mlango, wafanyakazi au watumishi wengine wa nyumba hii ya Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo hii ijulike kwenu, ya kuwa hakuna ruhusa kabisa ya kuwatoza kodi, wala ushuru wa forodhani wala wa njiani, walio watambikaji na Walawi na waimbaji na walinda malango na watumishi wa Nyumbani nao wengine wanaoitumikia Nyumba hiyo ya Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena twawaarifuni ya kuwa katika habari ya makuhani, na Walawi, na waimbaji, na mabawabu na Wanethini, au watumishi wa nyumba hii ya Mungu, si halali kuwatoza kodi, wala ada, wala ushuru.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tunawafahamisha tena kwamba inakatazwa kuwadai kodi ya mapato, malipo ya kuvuka mupaka na mengine makuhani, Walawi, waimbaji, walinzi wa mulango, wafanyakazi au watumishi wengine wa nyumba hii ya Mungu.