Ezra 7:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nawe Ezra, kwa kutumia hekima aliyokupa Mungu wako, hiyo uliyonayo, chagua mahakimu, na waamuzi watakaowaongoza wakazi wote wa mkoa wa magharibi ya Eufrate ambao wanaishi kufuatana na sheria ya Mungu wako. Na yule ambaye haijui sheria hiyo, mfundishe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nawe Ezra, kufuatana na hekima ya Mungu wenu uliyo nayo, weka mahakimu na waamuzi wote wanaozifahamu sheria za Mungu wenu, ili watoe haki kwa watu wote wa Ng’ambo ya Mto Frati. Nawe inakupasa umfundishe yeyote ambaye hazifahamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wewe, Ezra, kwa kadiri ya hekima ya Mungu wako iliyo mkononi mwako, waweke waamuzi na makadhi, watakaowahukumu watu wote walio ng'ambo ya Mto, yaani, wote wenye kuzijua amri za Mungu wako; ukamfundishe yeye asiyezijua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nawe Ezra, kwa kutumia hekima aliyokupa Mungu wako, hiyo uliyonayo, chagua mahakimu, na waamuzi watakaowaongoza wakazi wote wa mkoa wa magharibi ya Eufrate ambao wanaishi kufuatana na sheria ya Mungu wako. Na yule ambaye haijui sheria hiyo, mfundishe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nawe Ezra, kufuatana na hekima ya Mungu wenu uliyo nayo, weka mahakimu na waamuzi wote wanaozifahamu Sheria za Mungu wenu ili watoe haki kwa watu wote wa Ng'ambo ya Mto Eufrati. Nawe inakupasa umfundishe ye yote ambaye hazifahamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nawe Ezra, kufuatana na hekima ya Mungu wenu uliyo nayo, weka mahakimu na waamuzi wote wanaozifahamu sheria za Mungu wenu ili watoe haki kwa watu wote wa Ng’ambo ya Mto Frati. Nawe inakupasa umfundishe yeyote ambaye hazifahamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wewe, Ezra, kwa kadiri ya hekima ya Mungu wako iliyo mkononi mwako, waweke mahakimu na majaji, watakaowaamua watu wote walio ng'ambo ya Mto, yaani, wote wenye kuzijua amri za Mungu wako; na ukamfundishe yeye asiyezijua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nawe Ezra, kwa kutumia hekima aliyokupa Mungu wako, hiyo uliyonayo, chagua mahakimu, na waamuzi watakaowaongoza wakazi wote wa mkoa wa magharibi ya Eufrate ambao wanaishi kufuatana na sheria ya Mungu wako. Na yule ambaye haijui sheria hiyo, mfundishe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wewe Ezera kwa hivyo, unavyomjua Mungu wako kwa kweli, weka waamuzi na wenye kukata mashauri, wawakatie mashauri yao walio wa ukoo huu wote wanaokaa ng'ambo ya huko ya jito kubwa, wao wayajuao Maonyo ya Mungu wako, nao wasioyajua wawafundishe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wewe, Ezra, kwa kadiri ya hekima ya Mungu wako iliyo mkononi mwako, waweke waamuzi na makadhi, watakaowahukumu watu wote walio ng’ambo ya Mto, yaani, wote wenye kuzijua amri za Mungu wako; ukamfundishe yeye asiyezijua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nawe Ezra, kwa kutumia hekima Mungu wako aliyokupa, hiyo unayokuwa nayo, chagua wanasheria, na waamuzi watakaowaongoza wakaaji wote wa jimbo la upande wa magaribi wa muto Furati ambao wanaishi kufuatana na Sheria ya Mungu wako. Na yule ambaye haijui Sheria hiyo, umufundishe.