Ezra 7:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ezra aliondoka Babuloni, yeye alikuwa mwandishi mwenye ujuzi mwingi sana katika sheria ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, alikuwa amempatia Mose. Na kwa msaada wa Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, mfalme alimpatia Ezra kila kitu alichohitaji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huyu Ezra alipanda kutoka Babeli. Alikuwa mwandishi mwenye ujuzi mwingi katika Torati ya Musa, ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, alikuwa ametoa. Mfalme alikuwa amempa Ezra kila kitu alichoomba, kwa maana Mwenyezi Mungu, Mungu wake, alikuwa pamoja naye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
huyo Ezra akakwea kutoka Babeli; naye alikuwa mwandishi mwepesi katika sheria ya Musa, aliyokuwa ameitoa Bwana, Mungu wa Israeli; naye mfalme akamjalia matakwa yake yote, kama mkono wa Bwana, Mungu wake, ulivyokuwa pamoja naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ezra aliondoka Babuloni, yeye alikuwa mwandishi mwenye ujuzi mwingi sana katika sheria ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, alikuwa amempatia Mose. Na kwa msaada wa Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, mfalme alimpatia Ezra kila kitu alichohitaji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huyu Ezra alipanda kutoka Babeli. Alikuwa mwalimu mwenye ujuzi mzuri katika sheria ya Mose, ambayo BWANA, Mungu wa Israeli, alikuwa ametoa. Mfalme alikuwa amempa Ezra kila kitu alichoomba, kwa maana BWANA Mungu wake alikuwa pamoja naye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huyu Ezra alipanda kutoka Babeli. Alikuwa mwalimu mwenye ujuzi mzuri katika Torati ya Musa, ambayo bwana, Mungu wa Israeli, alikuwa ametoa. Mfalme alikuwa amempa Ezra kila kitu alichoomba, kwa maana bwana Mwenyezi Mungu wake alikuwa pamoja naye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
huyo Ezra akakwea kutoka Babeli; naye alikuwa mwandishi mwepesi katika Sheria ya Musa, aliyokuwa ameitoa BWANA, Mungu wa Israeli; naye mfalme akamjalia matakwa yake yote, kama mkono wa BWANA, Mungu wake, ulivyokuwa pamoja naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ezra aliondoka Babuloni, yeye alikuwa mwandishi mwenye ujuzi mwingi sana katika sheria ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, alikuwa amempatia Mose. Na kwa msaada wa Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, mfalme alimpatia Ezra kila kitu alichohitaji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyu Ezera akatoka Babeli, akapanda kuja kwao. Alikuwa mwandishi aliye fundi wa Maonyo ya Mose, Bwana Mungu wa Isiraeli aliyoyatoa; kwa kuwa mkono wa Bwana Mungu wake ulikuwa naye, mfalme akampa yote, aliyoyataka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
huyo Ezra akakwea kutoka Babeli; naye alikuwa mwandishi mwepesi katika sheria ya Musa, aliyokuwa ameitoa BWANA, Mungu wa Israeli; naye mfalme akamjalia matakwa yake yote, kama mkono wa BWANA, Mungu wake, ulivyokuwa pamoja naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ezra akaondoka Babeli, yeye alikuwa mwandishi mwenye ujuzi mwingi sana katika Sheria ambayo Yawe, Mungu wa Israeli, alikuwa amemupatia Musa. Na kwa musaada wa Yawe, Mungu wake, mufalme alimupatia Ezra kila kitu alichohitaji.