Ezra 8:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, nilitoa maagizo kuwa sote tufike karibu na mto Ahava ili tufunge na kujinyenyekeza mbele za Mungu wetu na kumwomba atulinde na kutuongoza katika safari yetu pamoja na watoto wetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kando ya Mto Ahava, hapo nilitangaza kufunga, ili tujinyenyekeze mbele za Mungu wetu na kumwomba kwa ajili ya kutujalia safari ya amani sisi na watoto wetu, pamoja na mali yetu yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo nikaamuru kufunga, hapo penye mto Ahava, ili tupate kujinyenyekeza mbele za Mungu, na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili yetu sisi wenyewe, na kwa ajili ya watoto wetu, na kwa mali yetu yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, nilitoa maagizo kuwa sote tufike karibu na mto Ahava ili tufunge na kujinyenyekeza mbele za Mungu wetu na kumwomba atulinde na kutuongoza katika safari yetu pamoja na watoto wetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kando ya Mto Ahava, hapo nilitangaza kufunga, ili tujinyenyekeshe mbele za Mungu wetu na kumwomba kwa ajili ya kutujalia safari ya amani sisi na watoto wetu, pamoja na mali zetu zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kando ya Mto Ahava, hapo nilitangaza kufunga, ili tujinyenyekeshe mbele za Mungu wetu na kumwomba kwa ajili ya kutujalia safari ya amani sisi na watoto wetu, pamoja na mali zetu zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo nikaamuru kufunga, hapo penye mto Ahava, ili tupate kujinyenyekeza mbele za Mungu, na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili yetu sisi wenyewe, na kwa ajili ya watoto wetu, na kwa mali yetu yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, nilitoa maagizo kuwa sote tufike karibu na mto Ahava ili tufunge na kujinyenyekeza mbele za Mungu wetu na kumwomba atulinde na kutuongoza katika safari yetu pamoja na watoto wetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo penye mto wa Ahawa nikatangaza mfungo, tujinyenyekeze mbele ya Mungu wetu na kumwomba, atuongoze sisi na watoto wetu na mali zetu zote kwenye njia inyokayo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo nikaamuru kufunga, hapo penye mto Ahava, ili tupate kujinyenyekeza mbele za Mungu, na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili yetu sisi wenyewe, na kwa ajili ya watoto wetu, na kwa mali yetu yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, nikatoa maagizo kuwa sisi wote tufike karibu na muto Ahara kusudi tufunge kula chakula na kujinyenyekeza mbele ya Mungu wetu na kumwomba atulinde na kutuongoza katika safari yetu pamoja na watoto wetu.