Ezra 8:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ingekuwa aibu kubwa kwangu kumwomba mfalme kikosi cha askari na wapandafarasi wa kutulinda na adui njiani maana nilikuwa nimekwisha mwambia kuwa Mungu wetu huwabariki wote wanaomtafuta, lakini huwachukia na kuwaadhibu wote wanaomwacha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Niliona aibu kumwomba mfalme askari na wapanda farasi wa kutulinda njiani kutokana na adui zetu, kwa sababu tulikwisha kumwambia mfalme, “Mkono wa neema wa Mungu wetu uko juu ya kila mmoja anayemtafuta, lakini hasira yake kubwa ni dhidi ya wote wamwachao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana naliona haya kumwomba mfalme kikosi cha askari na wapanda farasi, ili kutusaidia juu ya adui njiani; kwa maana tulikuwa tumesema na mfalme, tukinena, Mkono wa Mungu u juu ya watu wote wamtafutao, kuwatendea mema; bali uweza wake na ghadhabu yake ni kinyume cha wote wamwachao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ingekuwa aibu kubwa kwangu kumwomba mfalme kikosi cha askari na wapandafarasi wa kutulinda na adui njiani maana nilikuwa nimekwisha mwambia kuwa Mungu wetu huwabariki wote wanaomtafuta, lakini huwachukia na kuwaadhibu wote wanaomwacha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Niliona aibu kumwomba mfalme askari na wapanda farasi wa kutulinda njiani kutokana na adui zetu, kwa sababu tulikwisha kumwambia mfalme, “Mkono wa neema wa Mungu wetu uko juu ya kila mmoja anayemtafuta, lakini hasira yake kubwa ni dhidi ya wote wamwachao.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Niliona aibu kumwomba mfalme askari na wapanda farasi wa kutulinda njiani kutokana na adui zetu, kwa sababu tulikwisha kumwambia mfalme, “Mkono wa neema wa Mungu wetu uko juu ya kila mmoja anayemtafuta, lakini hasira yake kubwa ni dhidi ya wote wamwachao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana niliona haya kumwomba mfalme kikosi cha askari na wapanda farasi, ili kutusaidia juu ya adui njiani; kwa maana tulikuwa tumesema na mfalme, tukinena, Mkono wa Mungu u juu ya watu wote wamtafutao, kuwatendea mema; bali uweza wake na ghadhabu yake ni juu ya wote wamkataao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ingekuwa aibu kubwa kwangu kumwomba mfalme kikosi cha askari na wapandafarasi wa kutulinda na adui njiani maana nilikuwa nimekwisha mwambia kuwa Mungu wetu huwabariki wote wanaomtafuta, lakini huwachukia na kuwaadhibu wote wanaomwacha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani nalipatwa na soni za kumwomba mfalme, atupe kikosi cha askari na wenye kupanda farasi, watusaidie njiani kupigana na adui, kwa maana tulikuwa tumemwambia mfalme kwamba: Mkono wa Mungu wetu huwasimamia wote wamtafutao, uwapatie mema; lakini nguvu zake na makali yake huwatokea wote waliomwacha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana naliona haya kumwomba mfalme kikosi cha askari na wapanda farasi, ili kutusaidia juu ya adui njiani; kwa maana tulikuwa tumesema na mfalme, tukinena, Mkono wa Mungu u juu ya watu wote wamtafutao, kuwatendea mema; bali uweza wake na ghadhabu yake ni kinyume cha wote wamwachao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ingekuwa haya kubwa kwangu kumwomba mufalme kundi la waaskari na waaskari wapanda-farasi wa kutulinda na waadui katika njia maana nilikuwa nimekwisha kumwambia kwamba Mungu wetu anawabariki wote wanaomutafuta, lakini anawachukia na kuwaazibu wote wanaomwacha.