Ezra 8:28 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha nikawaambia, “Nyinyi ni wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Kadhalika vyombo ni wakfu na fedha na dhahabu ni matoleo ya hiari kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Niliwaambia, “Ninyi pamoja na vyombo hivi ni wakfu kwa Mwenyezi Mungu. Fedha na dhahabu ni sadaka ya hiari kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha nikawaambia, Ninyi mmekuwa watakatifu kwa Bwana, na hivyo vyombo ni vitakatifu; na fedha na dhahabu ni matoleo ya hiari kwa Bwana, Mungu wa baba zenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha nikawaambia, “Nyinyi ni wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Kadhalika vyombo ni wakfu na fedha na dhahabu ni matoleo ya hiari kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Niliwaambia, “Ninyi pamoja na vyombo hivi ni wakfu kwa BWANA. Fedha na dhahabu ni sadaka ya hiari kwa BWANA, Mungu wa baba zenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Niliwaambia, “Ninyi pamoja na vyombo hivi ni wakfu kwa bwana. Fedha na dhahabu ni sadaka ya hiari kwa bwana, Mungu wa baba zenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha nikawaambia, Ninyi mmekuwa watakatifu kwa BWANA, na hivyo vyombo ni vitakatifu; na fedha na dhahabu ni matoleo ya hiari kwa BWANA, Mungu wa baba zenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha nikawaambia, “Nyinyi ni wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Kadhalika vyombo ni wakfu na fedha na dhahabu ni matoleo ya hiari kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikawaambia: Ninyi m watakatifu wa Bwana, navyo hivi vyombo ni vitakatifu, nazo hizi fedha na dhahabu ni vipaji, alivyotolewa Bwana Mungu wa baba zenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha nikawaambia, Ninyi mmekuwa watakatifu kwa BWANA, na hivyo vyombo ni vitakatifu; na fedha na dhahabu ni matoleo ya hiari kwa BWANA, Mungu wa baba zenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha nikawaambia: “Ninyi mumetakaswa mbele ya Yawe. Vilevile na vyombo vimetakaswa na feza na zahabu ni matoleo ya mapenzi kwa Yawe, Mungu wa babu zenu.