Ezra 8:31 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnamo siku ya kumi na mbili ya mwezi wa kwanza, tulisafiri kutoka mto Ahava, kwenda Yerusalemu. Mungu wetu alikuwa pamoja nasi, akatulinda na maadui na washambuliaji wa njiani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tulianza safari kutoka Mto Ahava kwenda Yerusalemu siku ya kumi na mbili ya mwezi wa kwanza. Mkono wa Mungu wetu ulikuwa juu yetu, naye njiani alitulinda dhidi ya adui na wanyang’anyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo tukasafiri toka mtoni Ahava siku ya kumi na mbili ya mwezi wa kwanza, ili kwenda Yerusalemu; na mkono wa Mungu ulikuwa pamoja nasi, akatuokoa na mkono wa adui, na mtu mwenye kutuvizia njiani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnamo siku ya kumi na mbili ya mwezi wa kwanza, tulisafiri kutoka mto Ahava, kwenda Yerusalemu. Mungu wetu alikuwa pamoja nasi, akatulinda na maadui na washambuliaji wa njiani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tulianza safari kutoka Mto Ahava kwenda Yerusalemu kwenye siku ya kumi na mbili ya mwezi wa kwanza. Mkono wa Mungu wetu ulikuwa juu yetu, naye njiani alitulinda dhidi ya adui na wanyang'anyi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tulianza safari kutoka Mto Ahava kwenda Yerusalemu kwenye siku ya kumi na mbili ya mwezi wa kwanza. Mkono wa Mungu wetu ulikuwa juu yetu, naye njiani alitulinda dhidi ya adui na wanyang’anyi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo tukasafiri toka mtoni Ahava siku ya kumi na mbili ya mwezi wa kwanza, ili kwenda Yerusalemu; na mkono wa Mungu ulikuwa pamoja nasi, akatuokoa na mkono wa adui, na mtu mwenye kutuvizia njiani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnamo siku ya kumi na mbili ya mwezi wa kwanza, tulisafiri kutoka mto Ahava, kwenda Yerusalemu. Mungu wetu alikuwa pamoja nasi, akatulinda na maadui na washambuliaji wa njiani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha tukaondoka hapo penye mto wa Ahawa siku ya kumi na mbili ya mwezi wa kwanza kwenda Yerusalemu, nao mkono wa Mungu wetu ukatusimamia, ukatuokoa njiani mikononi mwa adui zetu namo mwao wanyang'anyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo tukasafiri toka mtoni Ahava siku ya kumi na mbili ya mwezi wa kwanza, ili kwenda Yerusalemu; na mkono wa Mungu ulikuwa pamoja nasi, akatuokoa na mkono wa adui, na mtu mwenye kutuvizia njiani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku ya kumi na mbili ya mwezi wa kwanza, tukasafiri kutokea kwenye muto Ahava, kwenda Yerusalema. Mungu wetu alikuwa pamoja nasi, akatulinda na waadui na washambulizi katika njia.