Ezra 8:35 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, watu wote waliorudi kutoka uhamishoni walimtolea Mungu wa Israeli sadaka zao za kuteketezwa. Walitoa mafahali 12 kwa ajili ya Israeli yote, kondoo madume 96 na wanakondoo 77; pia walitoa mbuzi 12 kama sadaka ya kuondoa dhambi. Wanyama wote hawa walitolewa kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha mateka waliokuwa wamerudi kutoka utumwani wakatoa sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa Mungu wa Israeli: mafahali kumi na wawili kwa ajili ya Israeli wote, kondoo dume tisini na sita, wana-kondoo sabini na saba, na beberu kumi na wawili kuwa sadaka ya dhambi. Hii yote ilikuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto kwa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wana wa uhamisho, waliokuwa wametoka katika uhamisho wakamtolea Mungu wa Israeli sadaka za kuteketezwa, ng'ombe kumi na wawili kwa ajili ya Israeli wote, na kondoo waume tisini na sita, na wana-kondoo sabini na saba, na mbuzi waume kumi na wawili, kuwa sadaka ya dhambi, hao wote pia walikuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, watu wote waliorudi kutoka uhamishoni walimtolea Mungu wa Israeli sadaka zao za kuteketezwa. Walitoa mafahali 12 kwa ajili ya Israeli yote, kondoo madume 96 na wanakondoo 77; pia walitoa mbuzi 12 kama sadaka ya kuondoa dhambi. Wanyama wote hawa walitolewa kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha mateka waliokuwa wamerudi kutoka utumwani wakatoa sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa Mungu wa Israeli: mafahali kumi na wawili kwa ajili ya Israeli wote, kondoo waume tisini na sita, wana-kondoo sabini na saba na mbuzi waume kumi na wawili kuwa sadaka ya dhambi. Hii yote ilikuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto kwa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha mateka waliokuwa wamerudi kutoka utumwani wakatoa sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa Mungu wa Israeli: mafahali kumi na wawili kwa ajili ya Israeli wote, kondoo dume tisini na sita, wana-kondoo sabini na saba na mbuzi dume kumi na wawili kuwa sadaka ya dhambi. Hii yote ilikuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto kwa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wana wa uhamisho, waliokuwa wametoka katika uhamisho wakamtolea Mungu wa Israeli sadaka za kuteketezwa, ng'ombe kumi na wawili kwa ajili ya Israeli wote, na kondoo dume tisini na sita, na wana-kondoo sabini na saba, na mabeberu kumi na wawili, kuwa sadaka ya dhambi, hao wote pia walikuwa sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, watu wote waliorudi kutoka uhamishoni walimtolea Mungu wa Israeli sadaka zao za kuteketezwa. Walitoa mafahali 12 kwa ajili ya Israeli yote, kondoo madume 96 na wanakondoo 77; pia walitoa mbuzi 12 kama sadaka ya kuondoa dhambi. Wanyama wote hawa walitolewa kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wao waliorudi kwenye uhamisho, walikopelekwa kwa kutekwa, wakamtolea Mungu wa Isiraeli ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima: ng'ombe dume 12 za Waisiraeli wote, madume ya kondoo 96, wana kondoo 77, tena madume ya kondoo 12 kuwa ng'ombe za tambiko za weuo; hawa wote wakawateketeza kuwa ng'ombe za tambiko za Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wana wa uhamisho, waliokuwa wametoka katika uhamisho wakamtolea Mungu wa Israeli sadaka za kuteketezwa, ng’ombe kumi na wawili kwa ajili ya Israeli wote, na kondoo waume tisini na sita, na wana-kondoo sabini na saba, na mbuzi waume kumi na wawili, kuwa sadaka ya dhambi, hao wote pia walikuwa sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, watu wote waliorudi kutoka katika uhamisho wakamutolea Mungu wa Israeli sadaka zao za kuteketezwa kwa moto. Wakatoa ngombe dume kumi na wawili kwa ajili ya Israeli yote, kondoo dume makumi kenda na sita na wana-kondoo makumi saba na saba; vilevile walitoa mbuzi kumi na wawili kama sadaka ya kusamehewa zambi. Nyama wote hawa walitolewa kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Yawe.