Ezra 8:36 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aidha, waliwakabidhi manaibu wa mfalme na watawala wa mkoa wa magharibi ya Eufrate mwongozo waliopewa na mfalme, nao walitoa msaada kwa watu na kwa ajili ya nyumba ya Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia walikabidhi manaibu wa mfalme na watawala wa Ng’ambo ya Mto Frati maagizo ya mfalme, ambao baadaye walitoa msaada kwa watu na kwa nyumba ya Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakawapa manaibu wa mfalme, na maliwali wa ng'ambo ya Mto, maagizo ya mfalme; nao wakawapa watu, na nyumba ya Mungu, msaada.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aidha, waliwakabidhi manaibu wa mfalme na watawala wa mkoa wa magharibi ya Eufrate mwongozo waliopewa na mfalme, nao walitoa msaada kwa watu na kwa ajili ya nyumba ya Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia walikabidhi manaibu wa kifalme na watawala wa Ng'ambo ya Mto Eufrati maagizo ya mfalme, ambao baadaye walitoa msaada kwa watu na kwa nyumba ya Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia walikabidhi manaibu wa mfalme na watawala wa Ng’ambo ya Mto Frati maagizo ya mfalme, ambao baadaye walitoa msaada kwa watu na kwa nyumba ya Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakawapa manaibu wa mfalme, na wakuu wa ng'ambo ya Mto, maagizo ya mfalme; nao wakawasaidia watu, na nyumba ya Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aidha, waliwakabidhi manaibu wa mfalme na watawala wa mkoa wa magharibi ya Eufrate mwongozo waliopewa na mfalme, nao walitoa msaada kwa watu na kwa ajili ya nyumba ya Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nazo zile amri za mfalme wakawapa watawala nchi wa mfalme na wenye amri waliozishika nchi za ng'ambo ya huku ya jito kubwa; kwa hiyo hawa wakawasaidia hawa watu katika kazi za Nyumba ya Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakawapa manaibu wa mfalme, na maliwali wa ng’ambo ya Mto, maagizo ya mfalme; nao wakawapa watu, na nyumba ya Mungu, msaada.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile wakawapa wasimamizi wa mufalme na watawala wa mukoa wa majimbo ya upande wa magaribi wa muto Furati maagizo waliyopewa na mufalme, nao wakatoa musaada kwa watu na kwa ajili ya nyumba ya Mungu.