Ezra 9:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wayahudi wanaoa wanawake wa kigeni na kuwaoza wavulana wao pia. Hivyo, taifa takatifu la Mungu limechanganyika na watu wa mataifa mengine Isitoshe, maofisa na wakuu ndio wa kwanza kutenda maovu hayo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wamewaoa baadhi ya binti zao kuwa wake zao na wake za wana wao, nao wamechanganya taifa takatifu na watu waliowazunguka. Nao viongozi na maafisa wamekuwa mstari wa mbele katika njia hii potovu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana wametwaa binti zao kuwa wake zao, na wake za watoto wao; basi mbegu takatifu wamejichanganya na watu wa nchi hizi; naam, mkono wa wakuu na mashehe umetangulia katika kosa hili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wayahudi wanaoa wanawake wa kigeni na kuwaoza wavulana wao pia. Hivyo, taifa takatifu la Mungu limechanganyika na watu wa mataifa mengine Isitoshe, maofisa na wakuu ndio wa kwanza kutenda maovu hayo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wamewaoa baadhi ya binti zao kuwa wake zao na wake za wana wao, nao wamechanganya taifa takatifu na watu waliowazunguka. Nao viongozi na maafisa wamekuwa mstari wa mbele katika njia hii potovu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wamewaoa baadhi ya binti zao kuwa wake zao na wake za wana wao, nao wamechanganya taifa takatifu na watu waliowazunguka. Nao viongozi na maafisa wamekuwa mstari wa mbele katika njia hii potovu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana wametwaa binti zao kuwa wake zao, na wake za watoto wao; basi mbegu takatifu wamejichanganya na watu wa nchi hizi; naam, mkono wa wakuu na viongozi umetangulia katika kosa hili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wayahudi wanaoa wanawake wa kigeni na kuwaoza wavulana wao pia. Hivyo, taifa takatifu la Mungu limechanganyika na watu wa mataifa mengine Isitoshe, maofisa na wakuu ndio wa kwanza kutenda maovu hayo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani wamejichukulia wenyewe na wana wao wanawake wa huko; ndivyo, walivyochanganya mazao matakatifu nayo yao ya makabila ya nchi hizi, nao wakuu wa watawalaji ndio walioanza kuinyosha mikono kuyavunja maagano ya Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana wametwaa binti zao kuwa wake zao, na wake za watoto wao; basi mbegu takatifu wamejichanganya na watu wa nchi hizi; naam, mkono wa wakuu na mashehe umetangulia katika kosa hili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wayuda wanaoa wanawake wa kigeni na kuwaoea wana wao vilevile. Hivyo, taifa takatifu la Mungu limechanganyika na watu wa mataifa mengine. Vilevile wasimamizi na wakubwa ndio wa kwanza kutenda maovu hayo.”