Ezra 9:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jioni, wakati wa kutoa tambiko ulipofika, niliinuka mahali hapo nilipokuwa nimekaa kwa huzuni huku nguo zangu zimeraruka pamoja na joho, nikapiga magoti na kumnyoshea mikono yangu Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, na kuomba,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo wakati wa kutoa dhabihu ya jioni nikainuka kutoka kujidhili kwangu nikiwa na koti na joho langu lililoraruka, nikapiga magoti mikono yangu ikiwa imeinuliwa kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wakati wa sadaka ya jioni nikainuka baada ya kunyenyekea kwangu, nguo yangu na joho yangu zimeraruliwa, nikaanguka magotini nikakunjua mikono yangu mbele za Bwana, Mungu wangu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jioni, wakati wa kutoa tambiko ulipofika, niliinuka mahali hapo nilipokuwa nimekaa kwa huzuni huku nguo zangu zimeraruka pamoja na joho, nikapiga magoti na kumnyoshea mikono yangu Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, na kuomba,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo wakati wa kutoa dhabihu ya jioni nikainuka kutoka katika kujidhili kwangu nikiwa na koti na joho langu lililoraruka, nikapiga magoti mikono yangu ikiwa imeinuliwa kwa BWANA Mungu wangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo wakati wa kutoa dhabihu ya jioni nikainuka kutoka kujidhili kwangu nikiwa na koti na joho langu lililoraruka, nikapiga magoti mikono yangu ikiwa imeinuliwa kwa bwana Mwenyezi Mungu wangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wakati wa sadaka ya jioni nikainuka baada ya kunyenyekea kwangu, nguo yangu na joho langu zimeraruliwa, nikaanguka magotini nikakunjua mikono yangu mbele za BWANA, Mungu wangu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jioni, wakati wa kutoa tambiko ulipofika, niliinuka mahali hapo nilipokuwa nimekaa kwa huzuni huku nguo zangu zimeraruka pamoja na joho, nikapiga magoti na kumnyoshea mikono yangu Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, na kuomba,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Saa ya tambiko ya jioni ilipofika, nikainuka hapo, nilipojinyenyekeza na kuzirarua nguo zangu na kanzu yangu, nikapiga magoti yangu, nikamkunjulia Bwana Mungu wangu mikono yangu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wakati wa sadaka ya jioni nikainuka baada ya kunyenyekea kwangu, nguo yangu na joho yangu zimeraruliwa, nikaanguka magotini nikakunjua mikono yangu mbele za BWANA, Mungu wangu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Magaribi, wakati wa kutoa sadaka ulipofika, nikasimama pahali pale nilipokuwa nimeikaa kwa huzuni nazo nguo zangu zimepasuka pamoja na koti, nikapiga magoti na kunyoosha mikono yangu kwa Yawe, Mungu wangu, na kuomba,