Ezra 9:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tangu nyakati za babu zetu hadi sasa, sisi watu wako tumekukosea sana. Na kwa sababu ya dhambi zetu, sisi, wafalme wetu na makuhani wetu tumetiwa mikononi mwa wafalme wa nchi za kigeni, tukauawa, tukachukuliwa mateka na kunyanganywa mali zetu. Na hadi hivi leo, tumetiwa haya kupita kiasi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tokea siku za babu zetu hadi sasa, hatia yetu imekuwa kubwa. Kwa sababu ya dhambi zetu, sisi na wafalme wetu na makuhani wetu tumekabiliwa na vita, utumwa, kutekwa na kudhiliwa katika mikono ya wafalme wa kigeni, kama ilivyo leo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tangu siku za baba zetu tumekuwa na hatia kupita kiasi hata leo; na kwa sababu ya maovu yetu sisi, na wafalme wetu, na makuhani wetu, tumetiwa katika mikono ya wafalme wa nchi hizi, tumepigwa kwa upanga, tumechukuliwa mateka, tumenyang'anywa mali zetu, tumetiwa haya nyuso zetu, kama hivi leo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tangu nyakati za babu zetu hadi sasa, sisi watu wako tumekukosea sana. Na kwa sababu ya dhambi zetu, sisi, wafalme wetu na makuhani wetu tumetiwa mikononi mwa wafalme wa nchi za kigeni, tukauawa, tukachukuliwa mateka na kunyang'anywa mali zetu. Na hadi hivi leo, tumetiwa haya kupita kiasi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tokea siku za babu zetu mpaka sasa, hatia yetu imekuwa kubwa. Kwa sababu ya dhambi zetu, sisi na wafalme wetu na makuhani wetu tumekabiliwa na vita, utumwa, kutekwa na kudhiliwa katika mikono ya wafalme wa kigeni, kama ilivyo leo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tokea siku za babu zetu mpaka sasa, hatia yetu imekuwa kubwa. Kwa sababu ya dhambi zetu, sisi na wafalme wetu na makuhani wetu tumekabiliwa na vita, utumwa, kutekwa na kudhiliwa katika mikono ya wafalme wa kigeni, kama ilivyo leo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tangu siku za baba zetu tumekuwa na hatia kupita kiasi hadi leo; na kwa sababu ya maovu yetu sisi, na wafalme wetu, na makuhani wetu, tumetiwa katika mikono ya wafalme wa nchi hizi, tumepigwa kwa upanga, tumechukuliwa mateka, tumenyang'anywa mali zetu, tumetiwa haya nyuso zetu, kama hivi leo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tangu nyakati za babu zetu hadi sasa, sisi watu wako tumekukosea sana. Na kwa sababu ya dhambi zetu, sisi, wafalme wetu na makuhani wetu tumetiwa mikononi mwa wafalme wa nchi za kigeni, tukauawa, tukachukuliwa mateka na kunyanganywa mali zetu. Na hadi hivi leo, tumetiwa haya kupita kiasi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tangu siku za baba zetu hata siku hii ya leo manza zetu sisi ni kubwa, kwa ajili ya hayo maovu yetu sisi na wafalme wetu na watambikaji wetu tulikuwa tumetiwa mikononi mwa wafalme wa nchi hizi, watuue kwa panga, watuteke, watunyang'anye mali zetu, watutukane usoni petu, kama vinavyofanywa hata leo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tangu siku za baba zetu tumekuwa na hatia kupita kiasi hata leo; na kwa sababu ya maovu yetu sisi, na wafalme wetu, na makuhani wetu, tumetiwa katika mikono ya wafalme wa nchi hizi, tumepigwa kwa upanga, tumechukuliwa mateka, tumenyang’anywa mali zetu, tumetiwa haya nyuso zetu, kama hivi leo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tangu nyakati za babu zetu mpaka sasa, sisi watu wako tumekukosea sana. Na kwa sababu ya zambi zetu, sisi, wafalme wetu na makuhani wetu tulitiwa katika mikono ya wafalme wa inchi za kigeni, tukauawa, tukapelekwa kuwa wafungwa na kunyanganywa mali zetu. Na hata hivi leo, tumetiwa haya kupita kiasi.