Ezra 9:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini sasa, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kwa muda mfupi umetuonesha huruma yako na kuwawezesha baadhi yetu kuponyoka kutoka utumwani na kuishi kwa usalama mahali hapa patakatifu. Badala ya utumwa, umetupa furaha na maisha mapya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Lakini sasa, kwa muda mfupi, Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, amekuwa na neema kwa kutuachia mabaki na kutupatia mahali imara katika mahali pake patakatifu, hivyo Mungu wetu anatupatia mwanga machoni petu na unafuu katika utumwa wetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na sasa kwa muda kidogo tumeneemeshwa na Bwana, Mungu wetu, hata akatuachia mabaki yaokoke, akatupa msumari katika mahali pake patakatifu. Mungu wetu atutie nuru machoni mwetu, tuburudike kidogo katika kufungwa kwetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini sasa, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kwa muda mfupi umetuonesha huruma yako na kuwawezesha baadhi yetu kuponyoka kutoka utumwani na kuishi kwa usalama mahali hapa patakatifu. Badala ya utumwa, umetupa furaha na maisha mapya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Lakini sasa, kwa muda mfupi, BWANA Mungu wetu amekuwa na neema kwa kutuachia mabaki na kutupa mahali imara katika mahali pake patakatifu, hivyo Mungu wetu atupa mwanga machoni petu na unafuu katika utumwa wetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Lakini sasa, kwa muda mfupi, bwana Mwenyezi Mungu wetu amekuwa na neema kwa kutuachia mabaki na kutupa mahali imara katika mahali pake patakatifu, hivyo Mungu wetu atupa mwanga machoni petu na unafuu katika utumwa wetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na sasa kwa muda kidogo tumeneemeshwa na BWANA, Mungu wetu, hata akatuachia mabaki yaokoke, akatupa msumari katika mahali pake patakatifu. Mungu wetu atutie nuru machoni mwetu, tuburudike kidogo katika kufungwa kwetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini sasa, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kwa muda mfupi umetuonesha huruma yako na kuwawezesha baadhi yetu kuponyoka kutoka utumwani na kuishi kwa usalama mahali hapa patakatifu. Badala ya utumwa, umetupa furaha na maisha mapya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa kitambo kidogo huruma imetutokea iliyotoka kwa Bwana Mungu wetu, akisaza kwetu wengine waliopona, tena akitupa kupigilia mambo mahali pake Patakatifu, Mungu wetu akitaka kuyaangaza macho yetu akitupa kupumua kidogo katika utumwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na sasa kwa muda kidogo tumeneemeshwa na BWANA, Mungu wetu, hata akatuachia mabaki yaokoke, akatupa msumari katika mahali pake patakatifu. Mungu wetu atutie nuru machoni mwetu, tuburudike kidogo katika kufungwa kwetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini sasa, ee Yawe, Mungu wetu, kwa muda mufupi umetuonyesha huruma yako na kuwawezesha wamoja kati yetu kuponyoka kutoka katika utumwa na kuishi kwa usalama pahali pako patakatifu. Pahali pa utumwa, umetupa furaha na maisha mapya.