Galatians 1:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa nataka kibali cha nani: Cha binadamu, ama cha Mungu? Au je, nataka kuwapendeza watu? Kama ningefanya hivyo, mimi singekuwa kamwe mtumishi wa Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, sasa mimi ninatafuta kukubaliwa na wanadamu au kukubaliwa na Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa bado najaribu kuwapendeza wanadamu, nisingekuwa mtumishi wa Al-Masihi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana, sasa je! Ni wanadamu ninaowashawishi, au Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sasa mnafikiri ninajaribu kuwapendeza wanadamu? Hapana, ninataka kumpendeza Mungu siyo wanadamu. Kama ningekuwa najaribu kuwapendeza wanadamu, nisingekuwa mtumwa wa Kristo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sasa nataka kibali cha nani: cha binadamu, ama cha Mungu? Au je, nataka kuwapendeza watu? Kama ningefanya hivyo, mimi singekuwa kamwe mtumishi wa Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa nataka kibali cha nani: cha binadamu, ama cha Mungu? Au je, nataka kuwapendeza watu? Kama ningefanya hivyo, mimi singekuwa kamwe mtumishi wa Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, sasa mimi ninatafuta kukubaliwa na wanadamu au kukubaliwa na Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa bado najaribu kuwapendeza wanadamu, nisingekuwa mtumishi wa Kristo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, sasa mimi ninatafuta kukubaliwa na wanadamu au kukubaliwa na Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa bado najaribu kuwapendeza wanadamu, nisingekuwa mtumishi wa Al-Masihi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana, sasa je! Ni wanadamu ninaowashawishi, au Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa nataka kibali cha nani: Cha binadamu, ama cha Mungu? Au je, nataka kuwapendeza watu? Kama ningefanya hivyo, mimi singekuwa kamwe mtumishi wa Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Hayo nayasemea kuitikiwa nao watu au naye Mungu? Au je? Natafuta kuwapendeza watu? Kama ningependeza watu bado, basi, singekuwa mtumwa wake Kristo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana, sasa je! Ni wanadamu ninaowashawishi, au Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi kusema vile inaonyesha kwamba ninatafuta watu wanikubali? Hapana! Ninataka kukubaliwa na Mungu. Au ninatafuta kuwapendeza watu? Kama ningekuwa ningali ninatafuta kuwapendeza watu, singekuwa mutumishi wa Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana sasa je! nawashawishi wana Adamu au Mungu? au nataka kuwapendeza wana Adamu? Kama ningekuwa hatta sasa nawapendeza wana Adamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.