Galatians 1:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndugu, napenda mfahamu kwamba ile Injili niliyoihubiri si ujumbe wa kibinadamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndugu zangu, nataka mjue kwamba Injili niliyowahubiria haikutokana na wanadamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana, ndugu zangu, injili hiyo niliyowahubiri, nawajulisha ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndugu zangu, ninawataka mjue kuwa ujumbe wa Habari Njema niliowaambia haukuandaliwa na mtu yeyote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndugu, napenda mfahamu kwamba ile Habari Njema niliyoihubiri si ujumbe wa kibinadamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndugu, napenda mfahamu kwamba ile Injili niliyoihubiri si ujumbe wa kibinadamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndugu zangu, nataka mjue kwamba Injili niliyowahubiria haikutokana na wanadamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndugu zangu, nataka mjue kwamba Injili niliyowahubiria haikutokana na wanadamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana, ndugu zangu, Injili hiyo niliyowahubiria, nawajulisha ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndugu, napenda mfahamu kwamba ile Injili niliyoihubiri si ujumbe wa kibinadamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndugu zangu, nawatambulisha, ya kuwa Utume mwema uliotangazwa nami sio wa kimtu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana, ndugu zangu, injili hiyo niliyowahubiri, nawajulisha ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wandugu zangu, ninawajulisha kwamba Habari Njema ninayohubiri haikutungwa na mutu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana injili biyo niliyowakhubiri nawajulisha, ndugu, ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu.