Galatians 1:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Bila shaka mlikwisha sikia jinsi nilivyokuwa ninaishi zamani kwa kuzingatia dini ya Kiyahudi, na jinsi nilivyolitesa kanisa la Mungu kupita kiasi na kutaka kuliharibu kabisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninyi mmekwisha kusikia kuhusu maisha yangu ya zamani nilipokuwa katika dini ya Kiyahudi, jinsi nilivyotesa makundi ya waumini wa Mungu kwa nguvu na kujaribu kuwaangamiza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana mmesikia habari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mmesikia juu ya mwenendo wangu hapo zamani nilipokuwa mfuasi hodari wa dini ya Kiyahudi. Nililitesa kwa nguvu kanisa la Mungu, nikiwa na shabaha ya kuliangamiza kabisa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Bila shaka mlikwisha sikia jinsi nilivyokuwa ninaishi zamani kwa kuzingatia dini ya Kiyahudi, na jinsi nilivyolitesa kanisa la Mungu kupita kiasi na kutaka kuliharibu kabisa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Bila shaka mlikwisha sikia jinsi nilivyokuwa ninaishi zamani kwa kuzingatia dini ya Kiyahudi, na jinsi nilivyolitesa kanisa la Mungu kupita kiasi na kutaka kuliharibu kabisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninyi mmekwisha kusikia juu ya maisha yangu ya zamani nilipokuwa katika dini ya Kiyahudi, jinsi nilivyolitesa Kanisa la Mungu kwa nguvu na kujaribu kuliangamiza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninyi mmekwisha kusikia juu ya maisha yangu ya zamani nilipokuwa katika dini ya Kiyahudi, jinsi nilivyolitesa makundi ya waumini wa Mungu kwa nguvu na kujaribu kuyaangamiza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana mmesikia habari za mwenendo wangu wa zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba nililitesa kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Bila shaka mlikwisha sikia jinsi nilivyokuwa ninaishi zamani kwa kuzingatia dini ya Kiyahudi, na jinsi nilivyolitesa kanisa la Mungu kupita kiasi na kutaka kuliharibu kabisa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mmesikia, nilivyoendelea hapo, nilipolifuata tambiko la Kiyuda, ya kuwa nalijipingia kuwafukuza wateule wa Mungu na kuwajengua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana mmesikia habari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mumesikia namna mwenendo wangu ulivyokuwa zamani, wakati nilipofuata dini ya Kiyuda. Munajua namna nilivyotesa kanisa la Mungu vikali sana na kujikaza kwa kuliharibu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana mmesikia khabari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi nikaliharibu,