Galatians 1:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naam, mimi niliwashinda wengi wa wananchi wenzangu wa rika langu katika kuizingatia dini ya Kiyahudi, nikajitahidi sana kuyashika mapokeo ya wazee wetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nami niliendelea sana katika dini ya Kiyahudi kuliko Wayahudi wengi wa rika langu, maana nilijitahidi sana katika desturi za baba zangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nilipata maendeleo makubwa katika dini ya Kiyahudi kwa kufanya kazi na kusoma kwa bidii kwa sababu nilikuwa mwaminifu kwa desturi za baba zetu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naam, mimi niliwashinda wengi wa wananchi wenzangu wa rika langu katika kuizingatia dini ya Kiyahudi, nikajitahidi sana kuyashika mapokeo ya wazee wetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naam, mimi niliwashinda wengi wa wananchi wenzangu wa rika langu katika kuizingatia dini ya Kiyahudi, nikajitahidi sana kuyashika mapokeo ya wazee wetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nami niliendelea sana katika dini ya Kiyahudi kuliko Wayahudi wengi wa rika yangu maana nilikuwa na bidii kubwa katika desturi za baba zangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nami niliendelea sana katika dini ya Kiyahudi kuliko Wayahudi wengi wa rika yangu maana nilijitahidi sana katika desturi za baba zangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami niliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naam, mimi niliwashinda wengi wa wananchi wenzangu wa rika langu katika kuizingatia dini ya Kiyahudi, nikajitahidi sana kuyashika mapokeo ya wazee wetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami hapo, nilipolifuata tambiko la Kiyuda, nikapita wenzangu wengi, ambao tulizaliwa nao mwaka mmoja, maana nilikaza kujihimiza, niandamane nayo, tuliyoyapokea kwa baba zetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nami niliendelea vizuri sana katika dini ya Kiyuda kuwapita watu wote wengine wa kabila langu wenye umri wangu, nikijikaza sana kushika desturi za babu zetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nami nalitangulia katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kushika mapokeo ya baba zangu.