Galatians 1:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara tu alipoamua kunifunulia Mwanawe kusudi niihubiri Habari Njema yake kwa watu wa mataifa mengine, bila kutafuta maoni ya binadamu,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
alimdhihirisha Mwanawe kwangu, ili nipate kumhubiri miongoni mwa watu wa Mataifa. Mimi sikushauriana na mwanadamu yeyote,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
kumfunua Mwanaye ili niweze kuwahubiri Habari Njema watu wasio Wayahudi. Hicho ndicho nilichofanya baada ya hapo. Sikuomba ushauri ama msaada wowote kutoka kwa mtu yeyote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mara tu alipoamua kunifunulia Mwanae kusudi niihubiri Habari Njema yake kwa watu wa mataifa mengine, bila kutafuta maoni ya binadamu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara tu alipoamua kunifunulia Mwanawe kusudi niihubiri Habari Njema yake kwa watu wa mataifa mengine, bila kutafuta maoni ya binadamu,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
alimdhihirisha Mwanawe kwangu, ili nipate kumhubiri miongoni mwa watu Mataifa. Mimi sikushauriana na mwanadamu ye yote,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
alimdhihirisha Mwanawe kwangu, ili nipate kumhubiri miongoni mwa watu wa Mataifa. Mimi sikushauriana na mwanadamu yeyote,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubirie Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara tu alipoamua kunifunulia Mwanawe kusudi niihubiri Habari Njema yake kwa watu wa mataifa mengine, bila kutafuta maoni ya binadamu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo, alipopendezwa kumfunua Mwana wake moyoni mwangu, kusudi nije, niwapigie wamizimu hiyo mbiu yake njema, papo hapo nikakata mawazo pasipo kuuliza mwili wangu ulio wenye nyama na damu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kumufunua Mwana wake kwangu, kusudi nihubiri Habari yake Njema kwa watu wa mataifa mengine. Na pale pale sikuomba shauri kwa mutu yeyote,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
alipoona vema kumdhihirisha Mwana wake ndani yangu, illi niwakhubiri mataifa khabari zake, marra sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu,