Galatians 1:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nashangaa kwamba muda mfupi tu umepita, nanyi mnamwasi Mungu aliyewaita kwa neema ya Kristo, na mnafuata injili ya namna nyingine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nashangaa kwamba mnamwacha upesi hivyo yeye aliyewaita kwa neema ya Al-Masihi na kuifuata Injili nyingine,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakati mfupi tu uliopita Mungu aliwaita mkamfuata. Aliwaita katika neema yake kwa njia ya Kristo. Lakini sasa nashangazwa kwamba kwa haraka hivi mmegeuka mbali na kuamini kitu kingine tofauti kabisa na Habari Njema tuliyowahubiri.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nashangaa kwamba muda mfupi tu umepita, nanyi mnamwasi yule aliyewaita kwa neema ya Kristo, mkafuata Habari Njema ya namna nyingine.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nashangaa kwamba muda mfupi tu umepita, nanyi mnamwasi Mungu aliyewaita kwa neema ya Kristo, na mnafuata injili ya namna nyingine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nashangaa kwamba mnamwacha upesi hivyo yeye aliyewaita kwa neema ya Kristo na kuifuata injili nyingine,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nashangaa kwamba mnamwacha upesi hivyo yeye aliyewaita kwa neema ya Al-Masihi na kuifuata Injili nyingine,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nashangaa kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia Injili ya namna nyingine.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nashangaa kwamba muda mfupi tu umepita, nanyi mnamwasi Mungu aliyewaita kwa neema ya Kristo, na mnafuata injili ya namna nyingine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nastaajabu, ya kuwa mwageuzwa upesi hivyo, mwondoke kwake yeye aliyewaita, mgawiwe kipaji chake Kristo, mkafuata utume mwema mwingine.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninashangaa sana kuona namna gani munageuka hivi upesi kwa kumwacha yule aliyewaita kwa njia ya neema ya Kristo na kufuata habari njema ya namna ingine.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nastaajabu kwa kuwa mmemwacha hivi upesi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo,