Galatians 1:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, hata kama mmoja wetu au malaika kutoka mbinguni, atawahubirieni injili tofauti na ile tuliyowahubirieni sisi, basi huyo na alaaniwe!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini hata ikiwa sisi au malaika atokaye mbinguni akihubiri Injili nyingine tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi mtu huyo alaaniwe milele!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tuliwahubiri ninyi ujumbe wa Habari Njema tu. Hivyo laana ya Mungu impate mtu yeyote yule anayewahubiri ninyi ujumbe ulio tofauti, hata ikiwa ni mmoja wetu au malaika kutoka mbinguni!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini, hata kama mmoja wetu au malaika kutoka mbinguni, atawahubirieni Habari Njema tofauti na ile tuliyowahubirieni sisi, basi huyo na alaaniwe!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, hata kama mmoja wetu au malaika kutoka mbinguni, atawahubirieni injili tofauti na ile tuliyowahubirieni sisi, basi huyo na alaaniwe!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini hata ikiwa sisi au malaika atokaye mbinguni akihubiri injili nyingine tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi mtu huyo alaaniwe milele!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini hata ikiwa sisi au malaika atokaye mbinguni akihubiri Injili nyingine tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi mtu huyo alaaniwe milele!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiria ninyi Injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiria, na alaaniwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, hata kama mmoja wetu au malaika kutoka mbinguni, atawahubirieni injili tofauti na ile tuliyowahubirieni sisi, basi huyo na alaaniwe!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini ikiwa sisi, au ijapo malaika wa mbinguni, akiwatangazia utume mwema mwingine kuliko ule, tuliowapigia sisi, na awe ameapizwa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kama sisi wenyewe au malaika kutoka mbinguni, akiwahubiri ninyi Habari Njema inayokuwa mbalimbali na ile tuliyowahubiri, alaaniwe!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini sisi au malaika wa mbinguni tukiwakhubiri ninyi injili illa hiyo tuliyowakhubiri, na alaaniwe.