Galatians 1:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tulikwisha sema, na sasa nasema tena: Kama mtu yeyote anawahubirieni injili ya aina nyingine, tofauti na ile mliyokwisha pokea, huyo na alaaniwe!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama vile tulivyokwisha kusema kabla, sasa nasema tena, ikiwa mtu yeyote atawahubiria Injili kinyume na ile mliyoipokea na alaaniwe milele!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nitalisema tena lile nililolisema hapo mwanzo. Ninyi mmekwishaipokea Habari Njema. Yeyote atakayewahubiri kitu kingine tofauti na ile Habari Njema mliyoipokea, basi mjue kwamba Mungu atamlaani mtu huyo!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tulikwisha sema, na sasa nasema tena: kama mtu yeyote anawahubirieni Habari Njema ya aina nyingine, tofauti na ile mliyokwisha pokea, huyo na alaaniwe!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tulikwisha sema, na sasa nasema tena: kama mtu yeyote anawahubirieni injili ya aina nyingine, tofauti na ile mliyokwisha pokea, huyo na alaaniwe!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama vile tulivyokwisha kusema kabla, sasa nasema tena, ikiwa mtu ye yote atawahubiria injili kinyume na ile mliyoipokea na alaaniwe milele!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama vile tulivyokwisha kusema kabla, sasa nasema tena, ikiwa mtu yeyote atawahubiria Injili kinyume na ile mliyoipokea na alaaniwe milele!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiria ninyi Injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tulikwisha sema, na sasa nasema tena: Kama mtu yeyote anawahubirieni injili ya aina nyingine, tofauti na ile mliyokwisha pokea, huyo na alaaniwe!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tuliyoyasema sasa hivi, narudia kuyasema tena: Mtu akiwatangazia utume mwema mwingine kuliko ule, mlioupokea, na awe ameapizwa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tumekwisha kuwaambia mambo haya zamani, nami ninayarudilia tena: mutu akiwahubiri habari njema inayokuwa mbalimbali na ile muliyopokea, alaaniwe!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, mtu awae yote akiwakhubiri injili illa hiyo tuliyowakhubiri, na alaaniwe.