Galatians 2:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Awali, kabla ya watu kadhaa waliokuwa wametumwa na Yakobo kuwasili hapo, Petro alikuwa akila pamoja na watu wa mataifa mengine. Lakini, baada ya hao watu kufika, aliacha kabisa kula pamoja na watu wa mataifa mengine, kwa kuogopa kikundi cha waliosisitiza tohara.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kabla baadhi ya watu waliotoka kwa Yakobo hawajafika, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa. Lakini hao watu walipofika alianza kujiondoa na kujitenga na watu wa Mataifa kwa sababu aliwaogopa wale wa kundi la tohara.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana kabla hawajaja watu kadha wa kadha waliotoka kwa Yakobo, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa; lakini walipokuja wao, akarudi nyuma akajitenga, huku akiwaogopa waliotahiriwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivi ndivyo ilivyotokea: Petro alipokuja Antiokia, hapo awali kabla ya Wayahudi kufika, alikula na kujumuika na wasio Wayahudi. Lakini baada ya Wayahudi kufika kutoka kwa Yakobo, Petro akajitenga na wasio Wayahudi. Akaacha kula pamoja nao kwa sababu aliwaogopa Wayahudi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Awali, kabla ya watu kadhaa waliokuwa wametumwa na Yakobo kuwasili hapo, Petro alikuwa akila pamoja na watu wa mataifa mengine. Lakini, baada ya hao watu kufika, aliacha kabisa kula pamoja na watu wa mataifa mengine, kwa kuogopa kikundi cha waliosisitiza tohara.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Awali, kabla ya watu kadhaa waliokuwa wametumwa na Yakobo kuwasili hapo, Petro alikuwa akila pamoja na watu wa mataifa mengine. Lakini, baada ya hao watu kufika, aliacha kabisa kula pamoja na watu wa mataifa mengine, kwa kuogopa kikundi cha waliosisitiza tohara.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kabla baadhi ya watu waliotoka kwa Yakobo hawajafika, alikuwa akila pamoja na watu Mataifa. Lakini hao watu walipofika alianza kujiondoa na kujitenga na watu Mataifa kwa sababu aliwaogopa wale wa kundi la tohara.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kabla baadhi ya watu waliotoka kwa Yakobo hawajafika, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa. Lakini hao watu walipofika alianza kujiondoa na kujitenga na watu wa Mataifa kwa sababu aliwaogopa wale wa kundi la tohara.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana kabla hawajaja watu kadhaa waliotoka kwa Yakobo, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa; lakini hao walipokuja, akarudi nyuma akajitenga, huku akiwaogopa waliotahiriwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Awali, kabla ya watu kadhaa waliokuwa wametumwa na Yakobo kuwasili hapo, Petro alikuwa akila pamoja na watu wa mataifa mengine. Lakini, baada ya hao watu kufika, aliacha kabisa kula pamoja na watu wa mataifa mengine, kwa kuogopa kikundi cha waliosisitiza tohara.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maana kulikuwako waliotumwa na Yakobo; hao walipokuwa hawajaja bado, alikula pamoja na wamizimu. Lakini walipokuja, akatoweka na kujitenga, kwani aliwaogopa wale waliotahiriwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana kabla hawajaja watu kadha wa kadha waliotoka kwa Yakobo, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa; lakini walipokuja wao, akarudi nyuma akajitenga, huku akiwaogopa waliotahiriwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana mbele ya kufika kwa watu wamoja waliotumwa na Yakobo kule, yeye alizoea kula pamoja na watu wa mataifa mengine. Lakini watu wale walipofika, akajitenga na kuacha kula pamoja na watu wa mataifa mengine, kwa sababu ya kuogopa wale wanaolazimisha kutahiriwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwa maana kabla hawajaja watu kadha wa kadha waliotoka kwa Yakobo, alikula pamoja na watu wa mataifa, illakini walipokuja akarudi nyuma akajitenga, akiwaogopa waliotahiriwa.