Galatians 2:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kweli, sisi kwa asili ni Wayahudi, na si watu wa mataifa mengine wenye dhambi!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sisi wenyewe ni Wayahudi kwa kuzaliwa na si watu wenye dhambi kama watu wa Mataifa,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sisi tulio Wayahudi kwa asili, wala si wakosaji wa Mataifa,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sisi ni Wayahudi kwa kuzaliwa. Hatukuzaliwa tukiwa ‘watenda dhambi’, kama vile Wayahudi wanavyowaita wale wasio Wayahudi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kweli, sisi kwa asili ni Wayahudi, na si watu wa mataifa mengine hao wenye dhambi!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kweli, sisi kwa asili ni Wayahudi, na si watu wa mataifa mengine wenye dhambi!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sisi wenyewe ni Wayahudi kwa kuzaliwa na si watu wenye dhambi kama watu Mataifa,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sisi wenyewe ni Wayahudi kwa kuzaliwa na si watu wenye dhambi kama watu wa Mataifa,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sisi tulio Wayahudi kwa asili, wala si wa Mataifa wenye dhambi,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kweli, sisi kwa asili ni Wayahudi, na si watu wa mataifa mengine wenye dhambi!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sisi tumezaliwa kuwa Wayuda, hatu wakosaji waliotoka kwao wamizimu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sisi tulio Wayahudi kwa asili, wala si wakosaji wa Mataifa,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hakika sisi Wayuda wa kizalikio hatuko watu wa mataifa mengine, hao wenye zambi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Sisi tulio Wayahudi kwa asili, wala si wenye dhambi wa mataifa,