Galatians 2:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa, ikiwa katika kutafuta tufanywe waadilifu kwa kuungana na Kristo sisi tunaonekana kuwa wenye dhambi, je, jambo hili lina maana kwamba Kristo anasaidia utendaji wa dhambi? Hata kidogo!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Lakini tukitafuta kuhesabiwa haki katika Al-Masihi, inakuwa dhahiri kwamba sisi ni wenye dhambi. Je, ina maana kwamba Al-Masihi amekuwa mtumishi wa dhambi? La hasha!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini ikiwa sisi wenyewe, kwa kutafuta kuhesabiwa haki katika Kristo, tulionekana kuwa wenye dhambi, je! Kristo amekuwa mtumishi wa dhambi? Hasha!
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa hiyo tunaamini uhusiano wetu kwa Kristo utatufanya tuhesabiwe haki mbele za Mungu. Ikiwa hiyo inatufanya tuonekane kama ‘watenda dhambi’ wasio Wayahudi, je itakuwa na maana kuwa Kristo anasababisha dhambi kuongezeka. Kwa hakika sivyo?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sasa, ikiwa katika kutafuta kukubaliwa kuwa waadilifu kwa kuungana na Kristo sisi tunaonekana kuwa wenye dhambi, je, jambo hili lina maana kwamba Kristo anasaidia utendaji wa dhambi? Hata kidogo!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa, ikiwa katika kutafuta tufanywe waadilifu kwa kuungana na Kristo sisi tunaonekana kuwa wenye dhambi, je, jambo hili lina maana kwamba Kristo anasaidia utendaji wa dhambi? Hata kidogo!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Lakini tukitafuta kuhesabiwa haki katika Kristo, inakuwa dhahiri kwamba sisi ni wenye dhambi, je, ina maana kwamba Kristo amekuwa mtumishi wa dhambi? La hasha!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Lakini tukitafuta kuhesabiwa haki katika Al-Masihi, inakuwa dhahiri kwamba sisi ni wenye dhambi. Je, ina maana kwamba Al-Masihi amekuwa mtumishi wa dhambi? La hasha!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini ikiwa sisi wenyewe, kwa kutafuta kuhesabiwa haki katika Kristo, tulionekana kuwa wenye dhambi, je! Kristo amekuwa mtumishi wa dhambi? La hasha!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa, ikiwa katika kutafuta tufanywe waadilifu kwa kuungana na Kristo sisi tunaonekana kuwa wenye dhambi, je, jambo hili lina maana kwamba Kristo anasaidia utendaji wa dhambi? Hata kidogo!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini sisi tunaotaka kupata wongofu kwa kuwa wake Kristo, sasa wenyewe tukionekana kuwa wakosaji, je? Kristo naye siye mwenye kutumikia makosa? La, sivyo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini ikiwa sisi wenyewe, kwa kutafuta kuhesabiwa haki katika Kristo, tulionekana kuwa wenye dhambi, je! Kristo amekuwa mtumishi wa dhambi? Hasha!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa tunapotafuta kuhesabiwa haki katika kuungana na Kristo, inaonekana kwamba sisi nasi ni wenye zambi sawa watu wa mataifa mengine. Jambo hili linaonyesha ya kama Kristo anatumika kwa ajili ya kuendelesha zambi? Hapana hata kidogo!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini kama sisi wenyewe tulipokuwa tukitafuta kufanyiziwa wema katika Kristo, tulionekana kuwa wenye dhambi, je! Kristo amekuwa mtumishi wa dhambi? Hasha.