Galatians 2:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini watu hawa wanaosemekana kuwa ni viongozi — kama kweli walikuwa hivyo au sivyo, kwangu si kitu, maana Mungu hahukumu kwa kuangalia mambo ya nje — watu hawa hawakuwa na mawazo ya kuniongezea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa habari ya wale waliokuwa wakubaliwe kuwa viongozi (kwangu mimi sikujali vyeo vyao, maana Mungu hana upendeleo), wale watu hawakuniongezea chochote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini wale wenye sifa ya kuwa wana cheo; (walivyokuwa vyo vyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa mwanadamu); nasema, hao wenye sifa hawakuniongezea kitu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na watu wale ambao walihesabiwa kuwa viongozi muhimu hawakuongeza lolote katika ujumbe wa Habari Njema niliyowahubiria watu. (Haijalishi kwangu kuwa walikuwa wa “muhimu” au la. Kwa Mungu binadamu wote ni sawa.)
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini watu hawa wanaosemekana kuwa ni viongozi—kama kweli walikuwa hivyo au sivyo, kwangu si kitu, maana Mungu hahukumu kwa kuangalia mambo ya nje—watu hawa hawakuwa na kitu cha kuongeza katika Habari hii Njema kama niihubirivyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini watu hawa wanaosemekana kuwa ni viongozi — kama kweli walikuwa hivyo au sivyo, kwangu si kitu, maana Mungu hahukumu kwa kuangalia mambo ya nje — watu hawa hawakuwa na mawazo ya kuniongezea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa habari ya wale waliokuwa wakubaliwe kuwa viongozi (kwangu mimi sikujali vyeo vyao, maana Mungu hana upendeleo), wale watu hawakuniongezea cho chote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa habari ya wale waliokuwa wakubaliwe kuwa viongozi (kwangu mimi sikujali vyeo vyao, maana Mungu hana upendeleo), wale watu hawakuniongezea chochote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini wale viongozi waliosifika kuwa wana cheo; (walivyokuwa vyovyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa mwanadamu); nasema, hao waliosifika hawakuniongezea kitu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini watu hawa wanaosemekana kuwa ni viongozi – kama kweli walikuwa hivyo au sivyo, kwangu si kitu, maana Mungu hahukumu kwa kuangalia mambo ya nje – watu hawa hawakuwa na mawazo ya kuniongezea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini waliowaziwa kuwa wenye cheo hivyo, walivyo kale, si kitu kwangu, maana Mungu hatazami uso wa mtu. Nasema: Nao hao walioambiwa kuwa wenye cheo hawakuniongezea jambo;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini wale wenye sifa ya kuwa wana cheo; (walivyokuwa vyo vyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa mwanadamu); nasema, hao wenye sifa hawakuniongezea kitu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kuelekea wale waliohesabiwa kuwa waongozi, hainifalii kitu kujua cheo gani walichokuwa nacho, kwa maana Mungu hahukumu kwa kuangalia mambo ya inje. Watu wale hawakunifundisha kitu kipya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini wale wenye sifa kwamba wana cheo, walivyo vyo vyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa mwana Adamu—nasema, wale wenye sifa hawakuniongezea kitu,