Galatians 2:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Badala yake, walitambua kwamba Mungu alikuwa amenituma kuhubiri Injili kwa watu wa mataifa mengine kama vile Petro alivyokuwa ametumwa kuihubiri kwa Wayahudi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Badala yake walitambua kwamba nilikuwa nimekabidhiwa kazi ya kuhubiri Injili kwa watu wa Mataifa, kama vile Petro alivyokabidhiwa kuhubiri Injili kwa Wayahudi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
bali, kinyume cha hayo, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa injili ya wasiotahiriwa, kama vile Petro ya waliotahiriwa;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini viongozi hawa waliona kuwa Mungu alinipa kazi maalumu ya kuhubiri Habari Njema kwa wasio Wayahudi, kama vile alivyomwagiza Petro kufanya kazi hiyo hiyo ya kuhubiri Habari Njema miongoni mwa Wayahudi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Badala yake, walitambua kwamba Mungu alikuwa amenituma kuhubiri Habari Njema kwa watu wa mataifa mengine kama vile Petro alivyokuwa ametumwa kuihubiri kwa Wayahudi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Badala yake, walitambua kwamba Mungu alikuwa amenituma kuhubiri Injili kwa watu wa mataifa mengine kama vile Petro alivyokuwa ametumwa kuihubiri kwa Wayahudi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Badala yake walitambua kwamba nilikuwa nimekabidhiwa kazi ya kuhubiri Injili kwa watu Mataifa, kama vile Petro alivyokabidhiwa kuhubiri Injili kwa Wayahudi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Badala yake walitambua kwamba nilikuwa nimekabidhiwa kazi ya kuhubiri Injili kwa watu wa Mataifa, kama vile Petro alivyokabidhiwa kuhubiri Injili kwa Wayahudi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
bali, kinyume cha hayo, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa Injili ya wasiotahiriwa, kama vile Petro alivyokabidhiwa ya waliotahiriwa;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Badala yake, walitambua kwamba Mungu alikuwa amenituma kuhubiri Injili kwa watu wa mataifa mengine kama vile Petro alivyokuwa ametumwa kuihubiri kwa Wayahudi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
lakini wakaona kweli, ya kuwa mimi nimepewa kuutangaza Utume mwema kwao wasiotahiriwa, kama Petero alivyopewa kuutangaza kwao waliotahiriwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
bali, kinyume cha hayo, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa injili ya wasiotahiriwa, kama vile Petro ya waliotahiriwa;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini walitambua kuwa Mungu amenipatia kazi ya kuhubiri Habari Njema kwa watu wa mataifa mengine sawa alivyomupatia Petro kazi ya kuihubiri kwa Wayuda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
bali, kinyume cha hayo, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa injili va wasiotahiriwa, kama vile Petro ya waliotahiriwa